Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Iringa ONESMO KAHOGGO amewataka viongozi katika Skimu za Umwagiliaji kusimamia kikamilifu zoezi la ukusanyaji ada na tozo kwa lengo la kutunisha mfuko wa Umwagiliaji. mwandishi wa matukio daima anaripoti kutokea Pawaga Iringa
Akizungumza mjini Iringa Mhandisi Kahoggo alisema endapo wakulima katika Skimu za Umwagiliaji watachangia fedha za ada ya usajili na matunzo kwa wakati, itasaidia kuharakisha ukarabati wa Skimu zilizoharibika kutokana na athari zitokanazo na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kujenga Skimu mpya nchini.
Alitolea mfano zoezi la kuurejesha mto Ruaha Mdogo katika njia yake ya asili limegharimu fedha kutoka mfuko wa umwagiliaji ambao unahitaji kuwezeshwa na wakulima hao.
Kwa upande wake Katalina Rashidi Mlaga mkulima mkazi wa kijiji cha Magozi aliishukuru serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kazi kubwa iliyofanywa ya kurejesha mto Ruaha Mdogo katika njia yake ya asili, nakusema kuwa wakulima katika kijiji hicho hutegemea zaidi kilimo cha umwagiliaji, na wamepata elimu ya kutosha kuhusu uchangiaji wa tozo za umwagiliaji na wapo tayari kuchangia.
Awali akiongea kijijini hapo Diwani wa kata ya Ilolo Mpya Funda Mihayo alimshukuru Mkurugenzi wa Tume ya taifa ya Umwagiliaji Daudi Kaali kwa kuwezesha wataalam wa tume kurekebisha miundombinu ya mifereji ya kupeleka maji katika mashamba ya wakulima pamoja na zoezi la usanifu linaloendelea katika Skimu ya Liganga ambapo lengo ni kuwezesha maji kunyweshea Skimu ya Magozi na Mkombilenga.
0 Comments