Basi la kampuni ya Isamilo lenye namba za usajili T 398 BNH YUTONG lililokuwa likitokea Mwanza limegongana na gari lori lenye namba T760BBY aina ya scani na kusababisha vifo vya watu wa nne na wengine wamejeruhiwa .
Kwa mujibu wa taarifa iliyothibitishwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Moyo ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Iringa alisema ajari hiyo ilitokea usiku wa jana OCTOBA 27 wakati basi hilo likitoka Mwanza kuelekea Iringa .
Moyo alisema ajali hiyo ilitokea kijiji cha Izazi kata ya Izazi tarafa ya Isimani wilayani Iringa katika barabara kuu ya Iringa -Dodoma .
Ambapo lori la kampuni ya Justas Investment Co limited likitokea Iringa likiendeshwa na dereva asiyefahamika aliyekimbia baada ya ajali liligongana na basi hilo mali ya Isamilo Supplies wa Mwanza.
Kuwa basi hilo lilikuwa likitoka Mwanza kwenda Mbeya lilikuwa likiendeshwa na dereva Emmanuel John Ng'wiguka (49) mkazi wa Buzuruga Mwanza .
Aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa mi Gerald John ambae ni dereva wa Mwanza,Happy Kwangu ambae ni utigo na mkazi wa Bunda,Edga ambae ni utingo mkazi wa Nyamongo Mara na abiria mmoja ambae bado hajafahamika jina jinsia ya kiume.
Huku majeruhi ni Ngeleja Mlima (36) mkazi wa Geita ,Allen Gahanga (21)Mkazi wa Mwanza,Sprime Kitanda (35) mkazi Igunga ,Fredrick Mgalula (36)mkazi wa Mafinga,Charles Mashauri (23)mkazi wa Mwanza,Novat Isaya (23)mkazi wa Igunga na Paulo Kayuki (25) mkazi wa Kalenga .
Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na majeruhi wanaendelea na matibabu katika Hospitali hiyo .
Pamoja na vifo na majeruhi hao pia ajali hiyo imesababisha uharibifu wa magari hayo .
Alisema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa Lori kujaribu kuyapita magari yaliyokuwa mbele bila kuchukua tahadhari na dereva huyo baada ya ajali alikimbia .
kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire amethibitisha kutokea Kwa ajali hiyo
0 Comments