Header Ads Widget

TAKUKURU YAJA NA MBINU MPYA

 

NA HADIJA OMARY MDTV LINDI 

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Lindi imeanzisha mpango wa Takukuru inayotembea itakayowawezesha kufahamu na kufanyia kazi kero mbali mbali za wananchi


 Akizungumza  na Waandishi wa Habari ofisini kwake na kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Taasisi hiyo,  kwa kipindi cha julay hadi Septemba 2021 Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Lindi Mhandis Abnery Mganga   amesema  kuwa,  kwa kutekeleza Mpango huo maafisa wa Takukuru huambatana na wakuu wa Idara za halmashauri ili kuweza kutatua kero za wananchi 


Alieleza kuwa katika Mpango huo wananchibwengi wamejitokeza na kulalamikia Matumizi mabaya ya Madaraka ya viongozi katika maeneo ya kata na vijiji ikiwemo kutopewa taarifa juu ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao pamoja na kutosomwa mapato na matumizi ya miradi inayosimamiwa na ngazi ya vijiji na kata.


Aidha alitaja mogogoro ya Aridhi isiyoisha, tozo Mbali mbali za Halmashauri,  kuchelewa kupata malipo ya mazao yao baada ya kuuzwa na ubadhirifu wa viongozi ni miongoni mwa kero kubwa walizozigundua katika ufuatiliaji huo


Hata hivyo Mganga ameeleza kuwa katika kipindi hiko jumala ya 81 yalipokelewa , kati ya hayo 48 yalihusu Rushwa na 33 hayakuhusu Rushwa ambapo alisema kuwa kati ya malalamiko hayo 48 yanayohusu rushwa yalifunguliwa majalada ya uchunguzi ambapo majarada 46 yanaendelea na majarada 2 yamekamilika huku taarifa 33 ambazo hazihusu Rushwa zikihamishiwa katika idara nyingine kwa hatua zaidi.


Mganga pia ameeleza  namna Taasisi hiyo ilivyojipanga katika kuendelea na kufuatilia miradi mbali mbali ya kimkakati kwenye Mkoa huo katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/2022 ikiwemo ya ujenzi wa Barabara vijijini, ujenzi wa Madarasa, Zahanati pamoja na Ujenzi wa Miundombinu ya Maji  tandangongoro 

Mwishooo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI