Header Ads Widget

SHULE 10 BORA KITAIFA MATOKEO YA DARASA LA SABA .,SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA YAONGOZA KIWILAYA

 



Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi 2021 (Matokeo ya Darasa la Saba mwaka 2021... Hii hapa orodha ya shule 10 bora kitaifa na 10 ambazo zimeongeza ufaulu kwa kiasi kikubwa kitaifa miaka mitatu mfululizo.
Wakati matokeo ya darasa la saba yaliyotangazwa leo yakipokelewa kwa hisia tofauti, Shule ya Msingi Graiyaki ya mkoani Mara ndiyo imeongoza kitaifa katika matokeo hayo huku Mkoa wa Kagera ukiongoza kuingiza shule nyingi katika orodha ya shule 10 bora kitaifa. 

Matokeo hayo ya mtihani huo uliofanyika Septemba mwaka huu yametangazwa leo Oktoba 30, 2021 na Baraza la Mtihani Tanzania (Necta) ambapo ufaulu wa ujumla umeongezeka kwa asilimia 6.6 ndani ya mwaka mmoja.

Watahiniwa 907,820 kati ya 1,107,460 waliofanya mtihani huo wamefaulu sawa na asilimia 81.97 ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 74,130 ikilinganishwa na mwaka jana.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde akitangaza matokeo hayo ameitaja Graiyaki ambayo ilikuwa na watahiniwa 50 kushika nafasi ya kwanza kitaifa ikifuatiwa na St Peter Claver ya mkoani Kagera katika nafasi ya pili.

Nafasi ya tatu imeenda kwa Shule ya Msingi Rocken Hill ya mkoani Sinyanga, Kemebos ya Kagera imeshika nafsi ya nne huku Bishop Caeser ya Kagera pia ikishika nafasi ya tano.
Shule ya Msingi Kwema Modern iliyokuwa na watahiniwa 44 ya Shinyanga iko nafasi ya sita, St Magret (Arusha) nafasi ya saba, Waja Springs (Geita) iko katika nafasi ya nane na Kadama ya Geita imeshika nafasi ya tisa.

10 bora hiyo imefungwa na Shule ya Msingi Chalinze Modern Islamic ya mkoani Pwani.
Kwa matokeo hayo, mkoa wa Kagera ndiyo umeingiza shule nyingi (3) ukifuatiwa na Shinyanga na Geita ambayo imeingiza shule mbili kila moja huku mikoa iliyobaki ikiingiza shule moja moja. Pia orodha hiyo imetawaliwa na shule kutoka Kanda ya Ziwa ambapo nane za kanda hiyo zimeingia.

Licha ya ushindani kuwa mkali kuwania orodha hiyo ya dhahabu, Graiyaki imefanikiwa kuvunja rekodi yake ya mwaka 2019 baada ya kuishusha Shule ya Msingi God’s Bridge ya mkoani Mbeya ambayo mwaka jana ilishika nafasi ya kwanza kitaifa.

Shule hiyo ya God’s Bridge haipo kabisa katika 10 bora ya mwaka huu wala Mbeya haijafanikiwa kuingiza shule hata moja katika orodha hiyo.

Shule hiyo imeshika nafasi ya 756 kati ya 11909 katika kundi lake la shule zisizozidi wanafunzi 50
Katika hatua nyingine, Shule ya Msingi Twiboki ya mkoani Mara ambayo mwaka huu imefanikiwa kutoa wanafunzi watano bora kitaifa, imetupwa nje katika orodha ya 10 bora ambayo katika matokeo ya mwaka jana ilishika nafasi ya tatu.
Wakati huo huo Uongozi wa shule ya Southern Highland iliyopo Mafinga Mkoani Iringa unawapongeza wanafunzi wake wote waliofanya mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka 2021 kwa kufaulu vizuri mtihani huo na kuendelea kuipa heshima iliyotukuka shule hiyo na imekuwa ya kwanza kiwilaya kwa mara nyingine tena.

kutokana na matokeo yaliyotangazwa leo, Shule ya Southern Highland imekuwa ya kwanza kiwilaya  kati ya shule 12 na ya 4 kimkoa kati ya shule 146 huku Kitaifa ikishika nafasi ya 144 kati ya shule 5664

Uongozi wa shule ulisema wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba walikuwa 32 huku wastani wa shule ni 246.8438 na kundi lake ni chini ya wanafunzi 40

Na katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo tarehe 30 Oktoba shule ya Southern jumla ya wanafunzi 21 wamefaulu kwa alama A huku wanafunzi 11 wamefaulu kwa alama B na hakuna mwanafunzi aliyepata C, D na E. 

Hivyo Uongozi unapenda kutoa shukrani na pongezi kwa wazazi pamoja na walezi kwa kuchagua  Southern highland kuwa shule bora kwa watoto wao na pia wamewakaribisha wazazi wengine wawalete watoto wao katika shule hiyo ili wapate elimu bora na malezi mazuri.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI