Header Ads Widget

SIDO YAJIPANGA KUKABILIANA NA MABADILIKO KWENYE VIWANDA VYA KUKAMUA MAFUTA YA CHIKICHI

 



Meneja wa SIDO mkoa wa Kigoma Gervas Richard  amesema kuwa shirika hilo limejipanga na liko tayari kuzalisha mashine nyingi zaidi kwaajili ya kukamulia mafuta ya chikichi.


Kauli hiyo ameitoa leo mbele ya watafiti wa zao la chikichi walipotembelea kiwanda hicho na kupata taarifa mbalimbali ambapo amesema kuwa wanatengeneza mashinde hizo kulingana na oda ya mteja wao.


Amesema kuwa mpaka sasa mahisaji sio makubwa sana hivyo wanaweza kuyamudu hata yakiongezeka bado uwezo wanao.


Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze kwa wingi ili waweze kupata mashine hizo na kujiajili wenyewe kwa vikundi  ama kwakuchukua mikopo ya mashine inayotolewa na taasisi hiyo.


“Kutokana na hamasa kubwa inayotolewa na serikali juu ya kuongeza uzalishaji wa zao la chikichi tunaamini kuwa hata uzalishaji ukamuani utaongezeka hivyo na sisi tumejipanga tayari kukabiliana na hali hiyo”


“Tumeambiwa mbegu mpya aina ya chikichi aina ya Tenera inauzalishaji mkubwa lakini inatoa mafuta mengi zaidi hii kwetu ni fursa ambayo tulikuwa tukiisubiri kwa muda mrefu tunaamini viwanda vitaongezeka na sisi tutapa wateja sio wakununua mashine tu hata wateja wa kutaka mafunzo mbalimbali namna ya kuongeza thamani ya zao la chikichi” alisema Richard


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI