Header Ads Widget

SHILINGI BILIONI 51 KUJENGA VITUO VYA KUTOLEA HAKI NCHINI

SERIKALI imetumia jumla ya shilingi Bilioni 51.45 kwa ajili ya kujenga majengo sita (6) ya kisasa ya vituo vya kutolea Haki. mwandishi wa matukio daima Hamida Ramadhan anaripoti kutokea Dodoma

Hayo yalibainishwa leo mkoani Dodoma na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Othuman Makungu wakati wa ziara ya watumishi wa mahakama kutoka Zanzibar kuja kujifunza na kutembelea majengo ambayo ni vituo vya kutolea haki.

Alisema kupitia ujenzi wa vituo hivyo vikubwa na vyakisasa mrundikano wa kesi kati vituo vya kutolea haki utapungua kwani sasa hakuna visingizio tena.

"Sasa hakuna visingizio vya   kesi kuchelewe kusomwa kupitia vituo hivi tunaimani kesi zote sitamalizwa kwa haraka na watu kupata haki zao bila upendeleo," alisema Jaji Makungu

Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa Mahakama Tanzania bara Gabriel Olesante alisema mahakama sio Muungano lakini tunapokuja kwenye suala la haki inatenda haki kwa wote huku akieleza ujio huo kwa watumishi kutoka mahakama ya Zanzibar ni moja ya kuonyesha Watanzania na Wazanzibar ni wamoja .

"Tuendelee kudumisha Muungano wetu kwa ajili ya urithi wa vizazi vyetu vya leo na kesho," alisema Olesante

Naye Mtendaji Mkuu wa Mahakama.Zanzibar Kai Mbaruk alisema kwa muda mrefu mahakama ya Zanzibar imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya nafasi ambapo baada ya kukamilika kwa ujenzi wa jengo la mahakama linalojengwa sasa itaondoa changamoto hiyo.

Alisema wamefanya ziara hiyo kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali hasa kwenye jengo jipya la mahakama ya Dodoma.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI