Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Ikiwa ni siku chache tangu kutokee vurugu katika soko la kariakoo Mtaa wa msimbazi kwa kile kichodaiwa ni wafanyabiashara ndogo ndogo (wamachinga) kupinga kuondolewa katika maeneo yao, Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) limemuomba Rais Samia Suluhu Hassan akutane na wamachinga ili wamueleze kero walizonazo ajue namna ya kuzifanyia kazi.
Ombi hilo limetolewa na Msemaji wa wamachinga soko la Kariakoo Masoud Chauka wakati akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, jijini Dar es es salaam wakati akitoa ufafanuzi kuhusu vurugu za wamachinga zilizotokea katika soko la Kariakoo hivi karibuni.
Amesema kuwa vurugu hizo zimekua zikifanywa na baadhi ya makundi ya watu wanaotumiwa kisiasa kwa lengo la kukwamisha juhudi za Serikali ya kuhamisha wamachinga ili waende katika maeneo yaliyopangwa na kwa ajili ya kufanyia biashara.
"Kuna vikundi vimekua vikizuia viongozi wa wamachinga wasitekeleze majukumu yao ya kuwahamisha wamachinga,na hawa watu wanatumiwa na baadhi ya wanasiasa ili kutukwamisha ,tunaiomba Serikali ituhakikishie ulinzi wetu" amesema Masoud.
Amesema kuwa, suluhu ya matatizo yao ni kukutana na Rais Samia ili wamueleze kero zao, kwani hata yale maeneo tuliopangiwa kufanya biashara mengine sio rafiki mfano eneo la jangwani halina mwingiliano wa watu wengi, hivyo pale biashara inakua ngumu sana.
Hata hivyo, amesema katika maeneo Serikali wanayoyatoa kwa ajili ya wamachinga hao, kwa vile baadhi yao sio rafiki ni vyema wakawapatia jengo la DDC lililopo kariakoo waweze kufanyia biashara zao ,pamoja na kuangalia Majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) yasiyokua na wakazi ili wawajengee masoko wafanye biashara zao.
Awali Makamu Mwenyekiti wa Shirikiko hilo, Steven Lusinde, amesisitiza kuwa viongozi wanatakiwa wawashirikishe machinga maeneo wanayotaka kwenda kuwaweka ili kuondoa sintofahamu, kwani mengine sio rafiki kutokana na sababu mbalimbali.





0 Comments