


- Amshukuru na Kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutatua kero za Maji DSM.
- Ashuhudia Shehena ya Vifaa vya kufikisha huduma ya maji kwa Wananchi.
- Asema Tsh Bilion 5.4 za Mradi wa Maji Mshikamano zinakwenda kumaliza tatizo la Maji Jimbo la Kibamba.
- Akabidhi hundi za Tsh Milion 232 Kama fidia kwa Wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo ametembelea na kukagua Shehena ya Vifaa vya kufikisha huduma ya maji kwa Wananchi ambapo ameonyesha kuridhishwa na jitiada za DAWASA Katika kushughulikia tatizo la upatikanaji wa maji Dar es salaam.
RC Makalla amesema hayo wakati wa ziara kwenye bohari ya Vifaa ya DAWASA ambapo pia amekabidhi hundi ya Shilingi Milioni 232 kwa wakazi 7 wa eneo la Mshikamano waliokubali kuacha maeneo yao kupisha Mradi wa Ujenzi wa Tank la Maji Mshikamano.
Akizungumza kuhusu Mradi huo ambao unagharimu kiasi Cha Shilingi bilioni 5.4, RC Makalla amewahakikishia Wananchi wa Jimbo la Kibamba kuwa kukamilika kwa Mradi huo kutaoa Fursa kwa kila mwananchi kupata huduma ya maji Safi na Salama.
Aidha RC Makalla amepongeza jitiada za Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan Katika kushughulikia na kupatia ufumbuzi kero ya Maji ambapo amesema ana imani ifikapo 2025 upatikanaji wa maji Dar es salaam utakuwa 100%.





0 Comments