

- Atembelea ofisini alipouwawa Mtendaji na kufika msibani kuwafariji wafiwa.
- Aagiza ofisi za Serikali ya Mtaa na Kata kuwa na Mgambo wakati wa kazi.
- Asema msako umefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa wawili.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesikitishwa na tukio la mauaji ya kinyama ya Afisa Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Msumi yaliyofanyika siku ya jana na kulielekeza Jeshi la Polisi kuhakikisha wote waliohusika kwenye mauaji hayo wanachukukiwa hatua kali za kisheria.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipotembelea ofisi ya Mtaa yalipofanyika mauaji hayo na Nyumbani kwa familia ya marehemu ambapo ametoa mkono wa pole.
Kutokana na mauaji hayo RC Makalla ameelekeza kila ofisi ya Mtaa na Kata kuwa na Mgambo kwaajili ya Kuimarisha ulinzi.
Aidha RC Makalla amekemea Matukio ya watu kulazimisha maamuzi ya haki kuwanufaisha na badala yake ametaka kila mmoja kufuata sheria.
Hata hivyo RC Makalla amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kufanya jitihada za haraka na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wa mauaji hayo na kuelekeza waliosalia wakamatwe.
Tukio la mauaji ya Afisa Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Msumi Kivini Moow limetokea siku ya jana likihusisha watuhumiwa watatu wanaosadikika kutekeleza mauaji hayo kwa sababu zinazohusishwa na Mgogoro wa Ardhi.





0 Comments