Header Ads Widget

RC MAKALLA AMUHAKIKISHIA RAIS SAMIA HAKUNA FEDHA YA MRADI ITAKAYOTUMIKA VIBAYA DSM





Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemuhakikishia Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa Mkoa huo umejipanga kuhakikisha kiasi Cha fedha kitakacholetwa kwenye Mkoa huo kupitia fedha zikizotolewa na IMF kwaajili ya mapambano dhidi ya Covid 19 kitatumika kwa kazi iliyokusudiwa *pasipo ubadhirifu


Akizungumza kwenye kikao kazi na Watendaji wa Wilaya za Mkoa huo, RC Makalla amesema tayari zimeundwa Kamati makini zenye wajumbe waadilifu na wachapa kazi watakaosimamia matumizi sahihi ya fedha hizo.


Aidha RC Makalla Kamati hizo zitasimamia hatua kwa hatua kila Miradi ya Ujenzi wa madarasa, maji na maboresho ya mazingira ya Machinga Jijini humo.


Pamoja na hayo RC Makalla amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na njema anayoifanya Katika kuwapatia Wananchi huduma Bora na utekelezaji waMiradi mingi na mikubwa ya Maendeleo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI