Header Ads Widget

NDEGE NDOGO YAPOTEA KATIKA PORI LA SELOUS TUNDURU RUVUMA IKIWA NA RUBANI .

 



Na Amon Mtega Tunduru.


NDEGE ndogo aina ya BatHawak yenye no za usajiri 5H-WXO inayomilikiwa na shirika lisilo la kiserikali la uhifadhi linalojulikana kwa jina la Protected Areas Management Solution Foundation (PAMS) imepotea wakati ikielekea kwenye pori la akiba Selous kanda ya Kingupila.


Akizungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake , Mkuu wa Wilaya ya Tunduru  Julias Mtatilo alisema kuwa ndege hiyo aina ya BatHawak inayorushwa na rubani Samweli Balina Gibuy imepotea Oktoba 18 mwaka huu majira ya saa 9.:09 jioni ikiwa inaelekea Pori la akiba la Selous.


Amesema kuwa ndege hiyo ambayo iliombwa na mamlaka ya usimamizi wa wanyama Pori Tanzania -TAWA kupitia shirika la uhifadhi la Frankfurt Zoologocal Society (FZS)kwa lengo la kwenda kusaidia katika zoezi linaloendelea la utafutaji wa Faru weusi katika pori la akiba la Selous.


"Muda mfupi baada ya kuruka ndege inadaiwa ilionekana na wachimbaji wa madini eneo la matuli na baadae wananchi wa Kijiji cha Kajima kilichopo katika Kata ya Jakika Tarafa ya Matemanga wilayani Tunduru ikielekea uelekeo wa Mashariki mwa Kijiji cha Kajima ambacho kinakadiliwa kuwa na umbali wa kilomita 26 kutoka uwanja wa ndege wa Matemanga ambapo ndege hiyo iliruka wakati wa kuondoka" amesema Mkuu huyo wa Wilaya Mtatilo.


Ameeleza  kuwa ndege hiyo ilitarajiwa kutuwa kingupira majira ya saa 11:30 alasili  hadi 12:09 jioni ambapo kwa bahati mbaya haikufika kingupira kama ilivyotarajiwa na ndipo mawasiliano ya kuulizia kwa pande zote mbili ilikotoka na inako kwenda yalianza.


Mtatilo amesema kuwa baada ya kujiridhisha kuwa ndege hiyo haikufika Kingupira na wala haijaonekana kwenye uwanja wa ndege wa Matemanga ambapo ndiko kuna ofisi za PAMS Foundation wafanyakazi wenzake Rubani Samwel walimjulisha Mkurugenzi wa shirika hilo ambaye mara baada ya kufahamishwa aliangalia kwenye "Spider track" ya ndege hiyo yenye uwezo wa kuonesha alikopita na ilipo ndege hiyo na kwamba Spider track ilionesha kuwa ndege hiyo ilikuwa uwanjani majira ya saa 7 mchana ambapo muda huo alikuwa anafanya majaribio kabla ya safari kuanza na baada ya kuruka akielekea Kingupira Pori la Akiba la Selous spider track haikuoneaha chochote.


Aidha amesema kuwa taarifa zilitolewa katika ngazi za mamlaka mbalimbali huku maandalizi ya utafutaji na uokozi yikiendelea ambapo kazi hiyo imefanyika kwa siku tano kwa kutumia jumla ya ndege tano Kati ya hizo nne za mabawa na moja ni helicopter wameamua kusimamia  zoezi hilo na kuwaomba wananchi na vyanzo vingine kuendelea kutafuta ndege hiyo na kwamba zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakaye fanikiwa kutoa taarifa ya ndege hiyo.


Akizungumza kwa niaba ya Familia ya Rubani Samweli Balina Gibuyi, kaka wa Rubani huyo Jani Killa amesema kuwa wamepokea kwa masikitiko makubwa sana kupotea kwa ndugu yao lakini kwa kushirikiana na shirika la PAMS na Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama wanahakikisha wanampata ndugu yao lakini pia kupatikana na ndege aliyokuwa anaitumia.



Kwa upande wake mratibu wa mradi wa uhifadhi wa Tembo Ruvuma kwenye shirika la PAMS Foundation   Osca Bakumbezi amesema kuwa tukio hilo la simanzi kwa sababu kwanza Rubani wao walikuwa wanafanyanae kazi muda wote na wameshirikiana nae kwenye kazi nyingi na kwamba hata kazi aliyokuwa anaenda kuifanya ni kazi ambayo ilikuwa na manufaa makubwa kwa Taifa na si vinginevyo.



Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI