Header Ads Widget

MADIWANI SIHA WAKERWA NA MIFUGO KUHARIBU BARABARA.

 


Na WILLIUM PAUL,  Siha.



MADIWANI wa Halmshauri ya Siha mkoani Kilimanjaro wamewataka watendaji wa vijiji kusimamia pamoja na kudhibiti mifugo inayopitishwa na kuharibu barabara zinazojengwa na serikali kwa kuweka utaratibu mzuri wa njia zatakazotumika kw ajili ya mifugo hiyo.


Hayo yalisemwa jana na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Siha Noel Mollel mara baada ya kikao cha baraza la madiwani cha kuwasilisha taarifa za maendeleo ya kata zao na kuibua changamoto zinazokabili maeneo yao.




Kutokana na changamoto hiyo aliagiza viongozi hao ngazi ya kijiji kusimamia matumizi sahihi ya barabara kwa kuzuia upitishaji mifugo  na badala yake watenge njia ya kupitisha mifugo (mapalio ).


Awali hoja hiyo iliibuliwa na diwani wa Kata ya Orumelili Lilian Mollel wakati akiwasilisha taarifa yake ya maendeleo kwenye Kata kutokana na kuwepo kwa uharibifu wa miundombinu ya barabara huku mifugo ikihusishwa kuwa moja ya chanzo.




Alisema katika kata hiyo miundombinu ya barabara imekua ikiharibika kila mara jambo ambalo linachangia kukwamisha juhudi za maendeleo ya wananchi.


"Changamoto ya miundombinu hii  ya barabara kutokuchongwa pamoja na kuwekwa moramu inasababisha vumbi kuwa kubwa,tunaomba serikali kupitia TARURA barabara hizi  ziwekwe moramu kabla kipindi cha mvua hakijaanza."Alisema 


Juma Jani ni diwani wa Kata ya Sanya juu alisema changamoto hiyo imekua  ikikumba kata yake kutokana na watu wanaowakodishia wafugaji mashamba ndiyo chanzo cha kusababisha tatizo hilo na kuomba Baraza la madiwani kuazimia hatua ambazo zitachukuliwa ili kunusuru miundombinu ya barabara.




Akizungumzia hoja hiyo Meneja wa TARURA Wilaya ya Siha Mhandisi Protasi Kawishe alikiri kuwepo kwa tatizo hilo  linalochangia uharibifu wa miundombinu ya barabara kupitisha mifugo yao huku akitaka wafugaji watumie njia za kupitisha mifugo todauti na barabara zinazochongwa na kuwekwa moramu ili kutunza barabara hizo.


Alisema wamekua wakichonga barabara na kushindilia lakini barabara hiyo hiyo inatumika kupitishia mifugo jambo ambalo linachangia kuaharibika kwa miundombinu hiyo.


"Barabara hizi zisipoitishia mifugo zinauwezo wa kudumu hadi miaka mitatu ndipo irudiwe tena lakini ikipitisha mifugo haiwezi kumaliza hata mwaka mmoja inakua ineshaharibika,tunajua mifugo ni muhimu lakini pia miundombinu ya barabara nayo tunaihitaji katika matumizi ya kila siku hivyo nawaomba wafugaji tushikiriane ili tufikie lengo moja la maendeleo ya Wilaya mkoa na taifa kw aujumla."Alisema

Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI