Header Ads Widget

Mwanahabari arejesha dola milioni 4 zilizofichwa nyumbani kwake


Mwandishi wa habari wa Zambia ametoa $ 4m (£ 3m) zilizopatikana nyumbani kwake mwezi uliopita kama sehemu ya makubaliano ya msamaha wa rushwa, maafisa wametangaza.

Margaret Chisela Musonda, anayejulikana pia kwa jina la Faith Musonda, pia amesalimisha nyumba yake iliyoko katika eneo la kifahari katika mji mkuu, Lusaka, ambapo kiasi hicho cha pesa za sarafu ya nchini humo na dola za Kimarekani zilipatikana.

Maafisa hawajafichua jinsi alivyopata pesa na ymakosa yake, lakini walisema alikuwa amekiri kosa.

Bi Musonda ni mwandishi wa habari mashuhuri ambaye aliwahi kuhudumu katika shirika la habari la serikali. Hajatoa maoni juu ya jambo hilo.

Katika taarifa, timu ya pamoja ya upelelezi ilisema kwamba makubaliano hayo yatamfanya Bi Musonda aepuke kesi za jinai.

Ilisema sheria inaruhusu serikali "kutoa msamaha kwa watuhumiwa katika hali fulani kwa masharti kwamba wanakubali makosa na kurudisha kile walichopata kimakosa kupitia vitendo vya rushwa".

Timu hiyo ilijumuisha maafisa kutoka Tume ya Kupambana na Rushwa, Huduma ya Polisi ya Zambia, Tume ya kupambana na Dawa za Kulevya na Kituo cha Ujasusi wa Kifedha.

Wazambia kwenye mitandao ya kijamii wameelezea mseto wa maoni kuhusu makubaliano hayo:

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI