Header Ads Widget

Mvulana auawa baada ya kuingia katika shule ya wasichana usiku


Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 17 kutoka Kenya amefariki kutokana na majeraha aliyopata wakati aliposhambuliwa baada ya kuingia kisiri katika shule ya wasichana, polisi wamesema.

Mwanafunzi huyo wa kidato cha nne alikuwa miongoni mwa wanafunzi sita ambao waliripotiwa kuingia kinyemela katika shule ya wasichana kaunti ya Kiambu ambayo ni jirani na mji mkuu wa Nairobi.

Maafisa wa polisi wanasema kwamba mwanafunzi huyo aliingia katika bweni la shule hiyo mwendo wa saa kumi alfajiri kabla ya kuonekana na baadhi ya wasichana ambao walipiga kamsa.

Hatua hiyo iliwavutia walinzi wa shule hiyo , wafanyakazi na mwalimu mkuu. Wavulana watano kati yao walitorokana kwa mujibu wa maafisa wa polisi , mvulana aliyesalia alivamiwa na wanafunzi na wafanyakazi wa shule hiyo.

‘’Walimpiga na kumfanya kupata majeraha ambayo yalitishia Maisha yake . Mvulana huyo baadaye alifariki’’ , idara ya jinai ilisema katika mtandao wake wa twitter.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI