Header Ads Widget

MSANII WA MZIKI WA DANSI FALLY IPUPA JUMA TANO HII KUKINUKISHA JIJINI MWANZA

 

NA CHAUSIKU SAID MDTV MWANZA

Mwanamziki maarufu nchin Kongo na muimbaji wa Muziki wa dansi na Rumba  Fally Ipupa kukinukisha kesho jijini Mwanza katika ukumbi wa fukwe za malaika

Akizungumza kwa niamba ya Fally Ipupa meneja Wake Madina Djobongue amesema kuwa Fally amejiandaa vizuri kwa kutoa burudani kwa wana Mwanza na Mikoa jirani wajiandae kwa kupata burudani nzuri.

Madina amesema hayo leo Oktoba 12, 2021alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari na kusema kuwa kilichomleta  Fally Tanzania ni kwa ajili ya kutoa burudani ambayo tayari ameanzia Dar es_ salam na sasa ni zamu ya Mwanza.

"Njooni mshuhudie burudani atakayoitoa Fally katika ukumbi wa fukwe za mailaka itakavyofaana na aijawahi tokea" alisema Madina.

Aidha kwa upande mwingine Meneja amewataja baadhi ya wasanii wa Tanzania  ambao Fally amekuwa akivutiwa nao ambao ni pamoja na Diamond,  Alikiba,  Nandy,  pamoja na Barnaba wakati akijibu swali aliloulizwa na Waandishi wa Habari.

Kwa upande wake mratibu wa kampuni ya prime time promotions waliomleta Fall Edward Lusaka amesema kuwa Fall amejipanga kutoa burudani nzuri na itakayomvutia kila mtu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI