Header Ads Widget

MSAKO MKALI KWA WATUMIAJI WA VING'ORA NA VIMULIMULI KATIKA MAGARI BILA KIBALI CHA SERIKALI

Jeshi la polisi Mkoani Mwanza kuanza msako mkali kwa magari ya wafanyabiashara na magari ya watu binafsi yanayotumia ving'ora pamoja na vimulimuli bila kibali cha serikali. mwandishi wa matukio daima Chausiku Said anaripoti kutokea Mwanza

Hayo yalielezwa na kamanda wa polisi Mkoani Mwanza Ramadhani Ng'anzi wakati akifungua wiki ya nenda kwa usalama barabarani na kutoa maagizo hayo kwa madereva, na wamiliki wa vyombo vya moto pamoja na watu wenye magari binafsi.

Ng'anzi alieleza kuwa kumekuwa na baadhi ya wamiliki na madereva wa magari kukiuka sheria za barabarani na kufunga ving'ora pamoja vimulimuli bila kuwa na vibali maalum kutoka serikalini.

Alisema kuwa sheria ya usalama barabarani inatambua baadhi ya magari yanayotakiwa kuwa na ving'ora na vimulimuli na sio kila gari linapaswa kuwa na mahitaji hayo.

"Gari tutakalo likuta  lina king'ora na vimulimuli bila kuwa na kibali maalum ni lazima tutalichukulia hatua kali za kisheria" alisema Ng'anzi

Aidha alieleza kuwa lengo kuu la kufanya ukaguzi katika vyombo vya moto ni kuona namna vinafanya kazi huku vikiwa vimekidhi vigezo vya kukaa barabarani na ambavyo havijakidhi vigezo kuondolewa kabisa.

Mwenyekiti wa usalama barabarani Mkoa wa Mwanza Fedinard Chacha alieleza kuwa kamati ya usalama barabarani imejipanga kupuguza ajali zote za barabarani pamoja na vifo visivyotarajiwa.

"Kila mwenye chombo cha moto apeleke kikakaguliwe na sio kupita njia za mkato ili tuweze kulinda Mkoa wetu dhidi ya ajali na kutokomeza kabisa"alisema Chacha.

Jekonia James ni mmoja wa madareva alisema kuwa madereva wengi hawajali kuhusu usalama barabarani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI