Header Ads Widget

MADEREVA WA MABASI YA ABIRIA WAONYWA KUFUTIWA LESENI

 


Na Rehema Abraham

Jeshi la polisi kitengo Cha usalama barabarani limesema kuwa halitasita kumchukulia hatua za kisheria dereva yeyote atakayebainika kuvunja Sheria za usalama barabarani.


Kamanda wa jeshi la polisi kikosi Cha usalama barabarani nchini  kamishna msaidizi  mwandamizi wa Polisi( SACP) wilbroad Mtafungwa amesema hayo  wakati akizungumza katika stendi ya kuu ya Moshi, na madereva wa mgari yaendayo mikoani,  mkoani Kilimanjaro .


Aidha amesema kuwa jeshi Hilo litaingia barabarani kwa nguvu zote kuhakikisha kuwa madereva wote wanafuata kanuni na Sheria zilizowekwa barabarani.


"Sasa hivi niwaambie Kama Kuna wa kwenda mahalamani wataenda,watakaoyozwa fain watalipa,wakifungiwa leseni watafungiwa lakini Sasa hivi tunachokifikiria sio kukufingia leseni ni tumakwenda kwenye utaratibu wa wa kufuata madaraja yako yote."Alisema.


Amesema kuwa katika kipindi Cha mwisho wa mwaka kumekuwepo na ongezeko la abiria ambapo watu wengi wamekuwa wakisafiri kutoka eneo moja kwenda jingine kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali hususani  kibiashara ambapo amewataka madereva hao kutoendesha vyombo hivyo Katika hali ya kuhatarisha maisha ya abiria.


Katika hatua nyingine amesema kuwa matukio mengi ya ajiali yanayotokea yanasababishwa na madereva kutokuwa na umakini na kutochukua tahadhari wakati wanaendesha vyombo hivyo.


"Nasema hivyo kwa sababu gani,tunapoingia mwishoni mwa mwaka baadhi ya madereva wamekuwa wakiendesha  kwa kuvunja Sheria za barabarani kwa kuendesha mwendo kasi,na bahati nzuri Sheria ipo wazi na swala la mwendo kasi limefafanuliwa kwa mujibu wa Sheria kwamba dereva unatakiwaa kwenda mwendo wa kasi usiozidi kilomita 80 kwa saa hasa kwa mabasi ya kubeba abiria"Alisema.


Hata hivyo amewataka madereva hao KUACHA kusingizia miezi ya mwisho wa mwaka kuwa ni mwezi wa abiria kupata ajali kwani wanazitafuta wenyewe kwa kufanya vitendo visivyofaa barabarani na kusema ajali inaweza kutokea wakati wowote lakini kinachotakiwa ni wao wenyewe kufuata Sheria , kanuni na taratibu zilizowekwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI