Mkoa wa Kilimanjaro umeelezwa kuwa na Tatizo la viriba tumbo kwa wanawake wenye umri wa kuzaa kuanzia miaka 15 mpaka 49 ambayo kwa sasa imefikia asilimia 49. mwandishi wa matukio daima Rehema Abraham anaripoti kutokea Kilimanjaro
Akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya chakula duniani yaliyohitimishwa katika viwanja vya Mandela mkoani Kilimanjaro waziri wa kilimo Prof.Adolf Mkenda, amesema kuwa hali hiyo ipo juu ukilinganisha na wastani wa kitaifa ambayo ni asilimia 31.7 .
Aidha amesema kuwa hali hiyo imetokana na sababu mbalimbali ikiwemo ulaji mbovu wa vyakula, kutokufanya mazoezi na kubadilika kwa mitindo ya maisha, Kama vile kula chipsi , vyakula vyenye wanga kwa wingi na nafaka zilizo kobolewa .
"Kwa hiyo basi niwasihi wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanazingatia ulaji bora kwani madhara yanayotokana na ulaji mbovu wa vyakula ni makubwa mno hasa katika nyenzo za kiuchumi "Alisema Mkenda.
Katika hatua nyingine amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wamedhamiria kutatua changamoto ya lishe kwa kuendelea kutekeleza mpango jumuishi wa kitaifa wa maswala ya lishe awamu ya kwanza ya mwaka 2021-2022 mpaka 2025-2026 .
"Mpango huu ambao nitauzindua Leo umeandaliwa na wadau wa sekta mbalimbali hapa nchini na taasisi zisizo za Serikali zinazotekeleza maswala ya lishe pamoja na wadau wa maendeleo"Alisema Mkenda.
Hata hivyo amesema mpango huo utawasaidia wadau wa sekta ya kilimo kuandaa mipango na afua mbalimbali za lishe zitakazotumika na kuleta matokeo chanya yatakayoboresha maswala ya lishe hapa nchini.
Kwa upande wa mwakilishi wa umoja wa mataifa UN amesema kuwa mifumo ya chakula ni muhimu kuchagua kuwa endelevu kwani Duniani kwa sasa tunakabiliwa na mabadiliko ya tabia ya nchi kwani kumekuwepo na ukame na maeneo mengine kumekuwepo na mafuriko ambayo yamesababisha kuwa na maafa ya maswala ya chakula na lishe.
"Tusisahau pia kuangalia maswala ya COVID 19 ambayo imekuwa janga la kitaifa na zaidi limewaathiri wapendwa wetu ambapo ukiondoa na haya mabadiliko ya tabia ya nchi kama ukame na hivyo kuongeza bei ya chakula sokoni na uzalishaji umepungua''. Alisema.





0 Comments