Header Ads Widget

MKAZI WA IRINGA AKUTWA AMEFARIKI NA MWILI WAKE KUTELEKEZWA

Mkazi wa mtaa wa Mtwivila B Manispaa ya Iringa  Rehema Ismail amekutwa amefariki na mwili wake ukiwa umetelekezwa  kando ya barabara inayounganisha mtwivila B na Mtwivila C

Akizungumza na matukio daima TV Mtendaji wa kata ya Mtwivila Thadei Mhanga, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa alipokea taarifa ya tukio hilo leo saa mbili tarehe 19 Oktoba siku ya ijumaa.

''mnamo saa mbili kama na dakika nilipokea taarifa kuwa kumetokea na tukio la mauwaji mtaa wa viziwi mtwivila C basi nikachukua pikipiki nikaja nikakuta kuna watu wachache kuangalia kweli ni tukia la mauwaji, hatua niliyochukua nikampigia msaidizi wa kituo Mwangosi, akasema nipo kwenye kikao tuma meseji, nikamwambia kuna tukio la mauaji akapiga nikamueleza akasema basi tunakuja, baadae nikampigia police operation officer akasema nipo jirani nakuja'' Alisema Mhanga

Hata hivyo baadhi ya wakazi wa mtaa huo wamehudhunishwa  na pia walielezea jinsi walivyoguswa na kifo cha Neema Ismail na kuiomba serikali iwasaidie kukata vitindi vyote vilivyopo maeneo hayo.

''hajawahi kuwa na ubaya wala kugombana na mtu hata siku moja kwakweli ni huzuni, tunaomba tu serikali iingilie kati itoe vitindi hivi kinguvu pawe mahali peupe kabisaa na ulinzi uwepo, itusaidie sisi wanawake wa mtwivila maana wanawake ni jeshi kubwa na ni wahangaikaji tunahangaika huku huku unarudi umechelewa kidogo unavamiwa'' Alisema jirani aliyefahamika kwa jina la Romana Kitosi

Hata hivyo Jeshi la polisi Manispaa ya Iringa walifika katika eneo la tukio na kuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi zaidi na kuwaomba wananchi wawe watulivu kwa kipindi hicho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI