Header Ads Widget

MKANDARASI MSHANA , MAPROFESA WA MKWAWA NA NGULANGWA WA CUF WAFUTIWA KESI YA UHUJUMU UCHUMI


Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF-Chama Cha Wananchi Mhandisi Mohamed Ngulangwa ni miongoni mwa washitakiwa sita ( 6) waliofutiwa Kesi ya Uhujumu Uchumi, Kesi Na. 6 ya 2018. Kesi hiyo iliyodumu kwa miaka 3 bila kusikilizwa kwa upelelezi kutokamilika ni miongoni mwa kesi nyingi zinazofutwa kufuatia agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kufuta kesi zote za kubambikiza. 


Kesi hiyo imefutwa Jumanne Oktoba 12, 2021 Mahakama Kuu Iringa.


Washitakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni :-


1. Eng. Godwin Mshana ( Mmiliki wa Kampuni ya Ujenzi ya MNM Engineering Services Limited);


2. Prof. Philemon Mushi ( aliyekuwa Mkuu wa Chuo Cha Mkwawa 2007- 2012);


3. Prof. John Machiwa ( aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo-Utawala 2009-2012);


4. Jackson Matandu ( Mjumbe Bodi ya Zabuni, 2010)


5. Jane Mpuya ( Mjumbe Bodi ya Zabuni 2010); na


6. Eng. Mohamed Ngulangwa ( Meneja Miliki na Mjumbe Bodi ya Zabuni, 2009-2012).


Mwezi Juni 2018 washitakiwa walifikishwa Mahakama Kuu Iringa wakituhumiwa kusababisha hasara ya bilioni 2.4 alizolipwa Mkandarasi MNM Engineering Services Limited kutokana na Mradi wa Ujenzi wa Ukumbi wa Mihadhara kwenye eneo la Chuo Kikuu cha Mkwawa, Iringa. 

Hata hivyo Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ukaguzi Maalum ( Special Audit) ya 2018 ilibainisha kwamba hakuna Fedha iliyopotea kwenye Mradi huo na kwamba Mkandarasi aliyeondolewa kazini (MNM Engineering Services Limited) alikuwa amelipwa pungufu ya fedha aliyostahili kulipwa mpaka aliposimamishwa kazi Julai 2017.  

Profesa Mushi na Profesa Machiwa waliondoka Mkwawa na kurudi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mei 2012 wakati Eng. Ngulangwa alihamia TANESCO Makao Makuu, Ubungo Januari 2013 kabla ya kuacha rasmi utumishi wa Umma 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu.  Hivyo wote hawakuwepo Mkwawa 2017 wakati wa mgogoro wa Kimkataba uliopelekea kusitishwa kwa Mkataba baina ya Chuo Kikuu cha Mkwawa na MNM Engineering Services Limited.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI