Na Hamida Ramadhan Dodoma
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais TAMISEMI Ummy Mwalimu amepiga marufuku wakuu wa mikoa na wakurugenzi kusafiri nje ya mikoa yao bila kibali kutoka kwa Rais,Makamu wa Rais au Waziri Mkuu lengo ni kuwataka wakuu hao kusimamia kwa ukaribu matumizi ya fedha ya mkopo wa Trilioni 1.3 uliotolewa na shirika la Fedha Duniani (IMF )kwaajili ya mapambano dhidi ya Uviko 19 na utekelezaji miradi ya maendeleo.
Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo Jijini Dodoma wakati akitoa maelekezo ya matumizi ya fedha hizo za IMF kwa upande wa mamlaka ya Serikali za Mitaa wamepatiwa jumla ya shilingi Bilioni 535.6 ambazo zimegawanywa katika maeneo matatu ikiwa ni pamoja na Elimu, Afya na Kuwawezesha wananchi kiuchumi.
" Naagigza hakuna mkuu wamkoa yoyote kusafiri bila kibali labda apate kibari kutoka kwa wakuu wetu wa nchi tunataka tusimimie vyema fedha hizi ili tukamilishe ile miradi yetu ya kimaendeleo kama Rais Samia Suluhu Hassan aliyoelekeza Oktoba 10 jijini hapa," amesema Waziri Ummy.
Pia amewata wakuu washule kusima fedha hizo kwa kujenga vyumba vya madarasa na zoezi hili lianze na kukamililika mara maoja .
" Naelekeza fedha zote
zinazokwenda kwenye elimu niawataka wakurugenzi na wakuu wa shule kuhakikisha mnasimamia ujenzi wa madarasa na vifaa vyake bikamilike kabla ya tarehe 15 Desemba 2021," Amesema Waziri Ummy
Kwa upande wa Afya amesema wanakwenda kusimika mitambo ya kisasa ya utoaji huduma za kibingwa ikiwemo mitambo ya X -ray Kwani kwa muda mrefu katika hosptali zote nchini kulikuwa na uhaba kubwa la vifaa hivyo
WANANCHI.
Akizungumzia kuhusu wananchia mesema upande wa wananchi amesema fedha hizo pia zinakwenda kuwawezesha wananchi kiuchumi kwani fesha hizo ziende kuboresha miundombinu kwenye maeneo ya wafanyabiashara pia .
Aidha amelekeza viongozi wote wa mikoa kuhakikisha wanaweka alama katika majengo yote yatakayojengwa kwa mkopo huo wa IMF ili kuonyesha utekelezaji wake kwa vitendo kwakua viongozi watakaoshindwa kufanya hivyo watapelejwa moja kwa moja TAKUKURU.
0 Comments