TIMU za soka za Kiswamba Eletronics na Wakulungwa zitakutana kwenye fainali ya michuano ya ya Polisi Uhalifu Haulipi Cup mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Bwawani Maili Moja Wilayani Kibaha.
Kiswamba Eletronics imefanikiwa kuingia fainali baada ya kuifunga timu ya Wagosi kwa magoli 3-1 huku Wakulungwa wakifikia hatua hiyo baada ya kuifunga Bodaboda kwa magoli 2-0.
Michezo hiyo inapigwa kwenye uwanja wa Bwawani Maili Moja Wilayani Kibaha Timu za Wagosi na Bodaboda zitacheza kutafuta mshindi wa tatu mchezo utakaochezwa kwenye uwanja huo huo siku ya Ijumaa.
Mshindi wa mashindano hayo anatarajiwa kupata ng'ombe na shilingi 100,000 mshindi wa pili atapata mbuzi na shilingi 100,000 huku mshindi wa tatu akitarajiwa kushikwa mkono.
0 Comments