Na Fatma Ally, MDTV Dar es Salaam
Diwani wa Kata ya Minazi Mirefu Godless Malisa amewaomba viongozi wa ngazi za juu kutoa ushirikiano kwa watendaji wa ngazi za chini ili kulinda maslahi ya wananchi pamoja na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika majukumu yake.
Wito huo ameutoa jijini Dar es Salaam mapema leo hii wakati alipokua akizungumza na waandishi ambapo amesema lengo la Rais ni kuhakikisha wananchi wanatatuliwa changamoto zao kupitia watendaji waliopo chini yake hivyo ni vyema kila mmoja kwa nafasi yake akawajibika katika kutekeleza maagizo ya Rais Samia kwa maslahi mapana ya nchi ya Tanzania.
"Kwa pamoja tukishirikiana sisi kama watendaji tuliochini ya Rais tuweza kutimiza malengo ya Rais ya kutatua kero za wananchi kupitia utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM"amesema Malisa.
Amesema kuwa, Rais ni Taasisi, na anafanya kazi na watu wengi wakiwemo viongozi mbalimbali hivyo ni vyema kuanzia watendaji wa Mtaa hadi Mkuu wa Mkoa wakasimama kumsaidia Rasi na sio kumkwamisha kwa kuzuia maendeleo yasifanyike. kuzuwa
Akizungumzia maendeleo ya kata hiyo, amesema bado kuna changamoto ya ukosefu wa kituo Cha Afya pamoja na Shule ya Msingi jambo ambalo limekua kero kubwa hasa kutokana na ukubwa na wakata hiyo na wananchi waliopo.
Amesema kuwa, kwa kushirikiana na wananchi wameanza kushangishana fedha kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili, ili kuleta maendeleo ambapo wameshaandika barua kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo ili kuomba eneo la kujenga vituo hivyo.
Pia wameomba magodauni ya sudeko kupitia katibu Mkuu wa wizara ya kilimo na endapo ombi hilo litakubaliwa litapelekea kupata eneo ambalo wanaweza kujenga shule au kituo cha afya kulingana na fedha ambazo watapata kwa haraka kutoka Serikali Kuu katika kutatua changamoto hizo mbili.
"Kata yetu ina changamoto ya kituo Cha Afya na pamoja na Shule ya Msingi, tumeomba pesa tukipewa kutoka Serikali Kuu tunaweza kuanza ujenzi wowote kati ya hivi vitu viwili, kwa sababu vyote ni muhimu itategemea pesa za ujenzi gani zitaingia mwanzo"amesema Malisa.
Katika hatua nyingine, Diwani huyo, amewaomba wakazi wa Kata hiyo kushirikiana naye katika masuala mbalimbali ili kuweza kuleta maendeleo ndani ya kata hiyo, kwani yeye peke yake hawezi kufanya kila kitu lazima washirikiane .
Kwa upande wa ulinzi na usalama Malisa amesema, katika ofisi za kata Diwani huyo wanapanga kwenda kumshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla kuweka utaratibu maalumu kwa wagambo ili kuweza kuondoa vitendo vya rushwa katika majukumu yao.
"Suala la ulinzi ni jambo la msingi sana, ndio maana tunataka tujenge kituo Cha Polisi ili Polisi jamii wawe wanaenda kuripoti kituoni, kuna vitendo viovu vimeanza kujitokeza hii yote imetokana na kukosekana kwa ulinzi kitoimarika"amesema Malisa.
0 Comments