Na Gift Mongi, Moshi
Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) mkoa wa Kilimanjaro imeyakamata magari 212 katika kipindi cha miezi mitatu yaani Julai hadi Septemba 2021 kutokana na makosa mbalimbali ya ukiukwaji sheria na kanuni za leseni za usafirishaji.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ofisini kwake mjini Moshi Ofisa mfawidhi wa LATRA mkoa wa Kilimanjaro Paul Nyello alisema mamlaka hiyo katika ukaguzi wa magari unaondelea wamefanikiwa kukamata magari 212 kwa makosa mbalimbali yaukiukwaji wa leseni za biashara.
"Katika hili zoezi la miezi mitatu magari 212 tuliyakamata na hii imetokana na ukiukwaji unaofanywa na wasafirishaji na hili zoezi naomba kuwahakikishia kuwa ni endelelevu lazima tusimamie sheria"alisema
Alisema kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikipokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi kuwepo tatizo la ukiukwaji wa sheria na kanuni katika baadhibya maeneo wanayopatiwa huduma za usafiri.
Alisema magari hayo yamekamatwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukatisha safari bila kufuata sheria,kuingia njia ambayo haziwahusu, kutoza nauli ambayo siyo halali tofauti na nauli elekezi pamoja na lugha chafu kwa abiria.
"Baada ya kuyakamata sheria za LATRA zipo wazi kabisa tulichokifanya ni kuyatoza faini kwa mujibu wa sheria zetu ili wamiliki au wasimamizi wajifunze na kufuata leseni inavyoelekeza na si vinginevyo"alisema
Hali kadhalika mamlaka hiyo pia imewaonya baadhi ya madereva wanaozidisha abaria ,wanatumia lugha chafu kwa abiria na kwamba watachukuliwa hatua za kisheria kwani ni kinyume cha sheria na kutoa wito kwa abiria kutoa taarifa pindi wanapoona matukio hayo.
Stella Ollomi mkazi wa Kibosho alisema gari ya kusafirishia abiria katika njia ya Kibosho-Moshi wamekuwa na kasumba ya kutoza nauli isivyo halali na kuiomba mamlaka hiyo kuweka nguvu ya ziada eneo hilo kwani wanaoumia ni wengi.
"Hawa LATRA wasibaki tu ofisini naomba waje kwa ajili ya uangalizi wa kina katika maeneo yetu haya maana tumelalamika sana ifike mahali watuondolee hii kadhia"alisema
Mwisho...






0 Comments