Header Ads Widget

WANANCHI WAENDELEA KUJITOKEZA KUCHANJWA CHANJO YA UVIKO 19



 NA HAMIDA RAMADHAN DODOMA 


SERIKALI imesema wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la kuchanja chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19 ambapo watu Milioni 1 wamechanja chanjo ya Jonson Jonson (JJ) huku watu 20000 wakiwa tayari wamesha chanja chanjo mpya ya Synopharm .


Sambamba na hilo imesema chanjo ya Synopharm ni chanjo ambayo mtu anatakiwa kuchanja mara mbili ndani ya siku 28 ili kinga yake iwe imara zaidi na ndio dozi kamili ya chanjo hiyo.


Akiongea leo katika kikao kati ya Wizara ya Afya Wizara ya Tamisemi na Mashirika yasiokuwa ya Serikali Profesa Abel Makubi Katibu Mkuu Wizara ya Afya amesema lengo la kikao hicho ni kushirikishana katika mikakati ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO 19.



" Hapa naomba kusisitiza kitu kwa wananchi kutorudia kuchanja chanjo mara mbili kama wewe umesha chanja chanjo ya Jonson Jonson usirudie tena kuchanja chanjo hii mpya ya Synopharm," amesisitiza Profesa Makubi.

 

Na kuongeza kusema"leo tuko hapa katika kikao hiki tumekutana na sekta zisizokuwa za kiserikali pamoja na NGos kwani wao wako tayari kushirikiana na serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo ya UVIKO 19 kwa kuhakikisha wanawahamasisha na kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa uchanjaji wa chanjo ya UVIKO 19," amesema .


Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Tamisemi anayeshughulikia Afya Dkt Grace Magembe amesema wao kama Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi wamedhamilia na kuhakikisha kazi ya uhamasishaji inakwenda vizuri 



" Sisi Tamisemi tunashughulikia watu wengi hivyo baada ya kufika kwa chanjo hapa nchini tuliandaa mpango shirikishi kwa kuongea na wakuu wa mikoa na viongozi wa dini kueleza wananchi umuhimu wa uchanaji wa chanjo ya UVIKO 19 na katika hili tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa,"


Na kuongeza"Mafanikio ya wananchi kuchanja chanjo ya UVIKO 19 yapo na yanaonekana kwa kutumia viongozi wa serikali Dini na viongozi wa kimila watu hawa maetusaidia na hatimaye wananchi wamejitokeza kuchanja," amesema Dkt Magembe..


Naye Lilian Badi Mwenyekiti wa Baraza la Taifa NGos amesema kama asasi za kirai wako tayari kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO 19.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI