Header Ads Widget

WIZARA YA AFYA YAAGIZA UCHUNGUZI VIDEO YA MGONJWA ALIYEPOSTIWA MTANDAONI

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kupitia kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya Bi. Catherine Sungura imewataka wananchi wawe watulivu kufuatia video inayozunguka mitandaoni kuhusu mgonjwa aliyefika Hospitali ya Mkoa wa Temeke kudai hakupata huduma stahiki huku watumishi wakiendelea na shughuli binafsi. mwandishi wa matukio daima Andrew Chale anaripoti kutokea Dar Es Salaam.

Ambapo video hiyo kwa mara ya kwanza ilipostiwa jana 22 Oktoba kwenye mtandao wa Kijamii maarufu wa Instagram wa Mwanadada Mtanzania anayeishi Marekani Mange Kimambi huku ikitazamwa na watu mbalimbali ambao pia walitoa maoni yao juu ya huduma na manyanyaso wayapata kwenye hospitali za Serikali hapa nchini.

Aidha, katika taarifa hiyo kutoka Wizara ya afya ilieleza kuwa:

"Wizara ya Afya imepokea na kusikiliza video inayozunguka mitandaoni kuhusu mgonjwa aliyefika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Jijini Dar es Salaam kudai hakupata huduma stahiki huku watumishi wakiendelea na shughuli binafsi. 

"Wizara imetoa maelekezo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam afuatilie na kuwasilisha taarifa. Tunaomba wananchi wawe watulivu wakati jambo hili likifanyiwa kazi." Ilieleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa, inaomba kuonana na ndugu wa mgonjwa ilikusaidia utatuzi wa suala hilo;

"Aidha, Wizara inaomba kupata mawasiliano ya mgonjwa au ndugu wa mgonjwa huyo aliyelalamika Ili kurahisisha ufuatiliaji wa kina na kumpata mlalamikaji." Ilimalizia taarifa hiyo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI