KARANI katika gereji ya mfanyabiashara Francis Mroso, Philemon Kazibira(64), ameieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, kwamba aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, alifika katika ofisi yao akidai kuwa ni Ofisa wa Usalama wa Taifa(TISS) anayeshughulika na ukusanyaji wa kodi.
Karani huyo ambaye ni shahidi wa nne wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Ole Sabaya na wenzake sita, alitoa madai hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Patricia Kisinda.
0 Comments