Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema ameshtakiwa nchini Ufaransa kwa kuhusika na jaribio la kumlaghai mwanasoka mwenzake Mathieu Valbuena kuhusiana na viddeo ya ngono iliyopatikana katika simu yake.
Amepuuza mashtaka dhidi yake na kukosa kufika mahakamani mjini Versailles.
Kesi hiyo ni ya kutoka Juni 2015, wakati wanasoka hao walikua katika kambi ya mazoezi huko Ufaransa.
Sakata hiyo iliyokumba soka ya Ufaransa ilifanya wachezaji wote wawili kupoteza nafasi zao.
Karim Benzema, 33, hata hiyo amerejea katika timu ya Ufaransa na kufungia bao Real Madrid mjini Kyiv Jumanne katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.
Amefunguliwa mashataka pamoja na wanaume wengine wanne kwa kujaribu kumtapeli Bw. Valbuena, ambaye aliambia mahakama kuwa soka ni maisha yake.
"Nilijua video hiyo ingelivujishwa maisha yangu yataathiriwa katika timu Ufaransa," alisema kulingana na waandishi wa habari.
Kesi juu ya video hiyo ya ngono ilianza mwaka 2015 wakati Valbuena, ambaye sasa ana miaka 37, kumuomba mtu huko Marseille, Axel Angot, kupakua yaliyomo kwenye simu yake ya rununu kwa kifaa kipya.
0 Comments