Header Ads Widget

KILOSA: BODABODA ALIYEPOTEA APATIKANA AMEFUKIWA KWENYE KIROBA

 

Na Matukio Daima Media, Morogoro

TUKIO la kutoweka kwa Hassan Selemani, mwenye umri wa miaka 24, mkazi wa Kijiji cha Maguha wilayani Kilosa mkoani Morogoro, limechukua sura mpya baada ya mwili wake kupatikana ukiwa umefukiwa ardhini ndani ya kiroba katika Kitongoji cha Shuleni, Kijiji cha Maguha.


Mwili wa kijana huyo aliyekuwa akijihusisha na shughuli za usafirishaji wa abiria kwa pikipiki maarufu kama bodaboda, ulipatikana majira ya saa moja usiku wa Novemba 18, 2026, baada ya siku tano za msako uliofanywa kufuatia kutoweka kwake.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, amesema Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu sita wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya kijana huyo, huku uchunguzi ukiendelea kubaini ukweli wa tukio hilo.


Kupatikana kwa mwili huo kumefuatia tukio la Hassan kutoweka Novemba 14, mwaka huu, baada ya kuondoka akiwa amembeba abiria mwanamke na kutorejea nyumbani, hali iliyozua wasiwasi kwa ndugu zake na wananchi wa maeneo ya Maguha na Mtumbatu.


Hofu iliongezeka zaidi baada ya pikipiki aliyokuwa akiitumia katika shughuli zake kupatikana bila yeye kuwepo, huku juhudi za kumtafuta zikiendelea bila mafanikio.


Katika kipindi hicho, hali ya taharuki ilijitokeza miongoni mwa wananchi, ambapo baadhi yao walifanya vitendo vya kujichukulia sheria mkononi kwa kuchoma moto nyumba za watu waliokuwa wakihusishwa na kutoweka kwa Hassan.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya, alitembelea maeneo ya Maguha na Mtumbatu Novemba 18, 2026, na kuwataka wananchi kuwa watulivu na kuepuka vitendo vya vurugu vinavyoweza kuhatarisha usalama wa watu na mali zao


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI