Header Ads Widget

MAMIA YA RAIA WA ETHIOPIA WAKIMBILIA KENYA BAADA YA MAPIGANO KUZUKA MPAKANI MOYALE

Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limesema limeanza kutoa misaada ya kibinadamu kwa familia zilizokimbilia nchini Kenya baada ya mapigano kuzuka katika mji wa Moyale, mpakani mwa Ethiopia.

Shirika hilo limesema awamu ya kwanza ya msaada huo inalenga kufikia kaya 1,000.

Mamia ya raia wa Ethiopia, wengi wao wakiwa wanawake, watoto na vijana, wamevuka kuingia nchini Kenya tangu mapigano kuzuka siku ya Jumatano.

Wakazi wa mji wa Moyale wamesema milio ya risasi ilikuwa bado inasikika upande wa Ethiopia hadi hapo jana.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI