Header Ads Widget

DARASA JANJA LAWAPA HAMASA WASICHANA KUSOMA SAYANSI

Na Samwel Mpogole: Mbeya.

Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imeendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa kutumia TEHAMA, hatua ambayo imeanza kuwapa hamasa wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari Garijembe kujifunza masomo ya sayansi.

Wanafunzi hao sasa wanatumia darasa janja lenye mfumo wa kidijitali unaowawezesha kupata vitabu na maudhui mbalimbali ya masomo kupitia kompyuta.

Mwanafunzi wa Kidato cha Pili, Warda Ibrahim, amesema darasa hilo limewasaidia kuelewa masomo ya sayansi kwa urahisi zaidi, tofauti na kutegemea ubao pekee.

Kwa upande wake, Mboni Barnaba amesema matumizi ya darasa hilo yanawapa fursa ya kujifunza sayansi kwa vitendo, huku yakiwajengea msingi wa kufikiria taaluma zinazohusiana na TEHAMA.

Walimu wa shule hiyo wameeleza kuwa teknolojia hiyo imeongeza ufanisi wa ufundishaji, kwa kuwa wanafunzi wanaweza kutumia picha, mifano na maudhui ya kidijitali wakati wa kujifunza.

Mwalimu wa TEHAMA, Meshack Mwaipopo, amesema mfumo huo pia unapunguza utegemezi wa matumizi ya chaki, huku kila mwanafunzi akiwa na akaunti inayomwezesha kupata vitabu vya kidijitali.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang’onda, ameipongeza Halmashauri kwa kuwekeza katika TEHAMA, akisema uwepo wa darasa hilo katika shule ya wasichana unaweza kuwa kichocheo cha kuongeza hamasa ya wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi na taaluma za teknolojia.

Kwa ujumla, darasa hilo linatajwa kuwa sehemu ya jitihada za kuboresha elimu kwa kutumia teknolojia na kuwajengea wanafunzi uwezo wa kukabiliana na mahitaji ya dunia ya kidijit

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI