Header Ads Widget

ANDREW CHALE AFANYA TUKIO KUBWA LA KIHISTORIA NDANI YA NGORONGORO, ASHEREKEA BIRTHDAY NA WATOTO WA SHALOM


Na Matukio Daima Media

Karatu - Ngorongoro. Mdau na mwanahabari wa utalii, uhifadhi na Mazingira, Andrew Chale, ameandika historia kwa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa 21 Oktoba ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro, akiwa na Watoto wa kituo cha Watoto Shalom - Karatu, katika kutimiza miaka 41.

Tukio hilo lililopewa kauli mbiu ya 'Karibu Nyumbani sherekea na Ngorongoro' limewezeshwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). 

Shughuli zimefanyika katika Makumbusho ya Olduvai Gorge ambako watoto wamejifunza historia ya chimbuko la binadamu na ndani ya Bonde la Ngorongoro kushuhudia wanyamapori.

Ndani ya Bonde hilo, watoto wameshuhudia wanyamapori mbalimbali akiwemo Simba, Tembo, Faru Mweusi, Nyati na Twiga, huku wakipata elimu ya uhifadhi na utalii endelevu.

Akizungumza baada ya tukio hilo, Chale ameishukuru NCAA na kutoa wito kwa Watanzania kutumia vivutio vya ndani kusherekea mafanikio.

"Shukrani za kipekee kwa NCAA kwa kuwezesha tukio hili. Nitoe wito kwa Watanzania, tunaposherekea siku za kuzaliwa ama mafanikio basi tutumie vivutio vyetu vya ndani, hususani Ngorongoro". amesema Chale.

Mbali na ziara hiyo, Chale pia ametoa zawadi katika Kituo cha Shalom Orphanage Centre na amekuwa na utaratibu wa kila mwaka wa kusherekea siku yake hiyo ya kuzaliwa na watoto wenye mahitaji maalum sehemu mbalimbali nchini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI