Matukio Daima Media App, Dar es salaam.
KAMPUNI ya Zara Tanzania Adventures imefanikiwa kuzindua msimu wa tano wa kampeni ya "Twenzetu kileleni 2026" Ikiwa na lengo kuu kupanda mlima Kilimanjaro na kusheherekea miaka 65 ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania).
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi uliofanyika leo September 10, 2026 katika Chuo cha Taifa cha Utalii (National College of Tourism), Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Zara Tanzania Adventure, Bi. Zainabu Ansell 'Mama Zara' amesema kampeni hiyo inatarajiwa kuwashirikisha zaidi ya Watalii 200 mwaka huu, wote wakipanda Mlima Kilimanjaro kwenye njia ya Marangu kwa ajili ya kusherehekea Uhuru, 9 Desemba.
Mama Zara amesema wa tano, ikiwa na dhamira ya kuhamasisha Watanzania kusafiri, kugundua na kujivunia utajiri wa asili na vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania ambapo watapanda kwa bei nafuu kwa kiwango Cha Tsh 1,800,000 (Milioni 1.8) ambapo imejumlisha vitu vyote malazi, chakula, vifaa, usafiri na tozo Serikali.
Zoezi hilo la kupanda Mlima Kilimanjaro linatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 5 hadi Desemba 10, 2026, likiwa pia ni sehemu ya kuendelea kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, hususani Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Aidha, mbali ya kuzindua twenzetu kileleni msimu wa Tano, ZARA pia wamezindua Twenzetu Serengeti kwa matukio ya Utalii msimu mzima wa December.
Tutakuwa na safari ya kuanzia Springlands hotel Mjini Moshi, kwa gharama ya Tsh 1,200,000 (Milioni 1.2), gharama kwa kila mtu, safari ya siku Nne.
"Twenzetu Serengeti itajumlisha usafiri wa Land cruiser 4x4, chakula,vinywaji laini, malazi, viingilio vya Hifadhi. Kwa wageni kila gari watu 7.".
Katika uzinduzi huo wadau mbalimbali wameweza kushiriki akiwemo Bodi ya Utalii (TTB), kampuni ya simu ya TTCL, TISEZA, kampuni ya bima ya BUMACO, MSD, Chuo cha Utalii cha Taifa, na wengine wengi.









0 Comments