Na Matukio Daima Media.
Licha ya mkoa wa Njombe kutotajwa kwenye Mikoa itakayokumbwa na janga la mvua kubwa na za hatari za El nino,chama cha msalaba mwekundu Red cross kimeenza kuchukua hatua za kuwaelimisha wanachama wake ili waweze kukabiliana na janga lolote litakalotokea.
Ukiwa wilayani Makete uongozi wa Red cros mkoa ukiongozwa na Mwenyekiti wake Edgar Mtitu wakati ukijitambulisha baada ya uchaguzi umesema suala la kujitolea kukabiliana na maafa ni la kila mmoja bila kujali itikadi za kidini,Siasa wala kabila hivyo Wajibu wao ni kuchukua hatua wakati wowote pahala popote.
Aidha mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Mhe.Rabson Mahenge amesema kuanza mapema maandalizi ya mvua hizo kutasaidia sana kupunguza baadhi ya madhara kwani hata kama mkoa wa Njombe haujatajwa kukumbwa na mvua hizo lakini lazima kuna athari zitaweza kutokea ambazo ni Red cross itapaswa kuwajibika.
Akieleza majukumu ya Redcros mratibu wa Chama hicho mkoa wa Njombe Cyprian Madege amesema pamoja na kukabiliana na maafa mbalimbali lakini wanaowajibu wa kuziunganisha jamii pamoja.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Makete Kissa Kasongwa amewataka wanaredcross wilayani humo kuwa na moyo wa kujitolea na kufanya matendo ya huruma kwani hiyo ndiyo dini ya kweli.
Wakazi wa Makete ambao ni wanachama wa Redcros akiwemo Wilson Fungo wamesema maafa yamekuwa yakitokea katika maeneo mengi ndani ya wilaya hiyo hivyo wanaomba elimu hiyo ifike kila eneo pamoja na vifaa vya uokozi wakati wa majanga.
Baada ya mkutano huo uongozi wa red cros mkoa umetoa mahitaji mbalimbali kwa wahitaji wakiwemo wazee na wanafunzi.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)




0 Comments