Header Ads Widget

WHITEDENT WAGUSA AFYA YA KINYWA NA MENO MUHIMBILI KWA MSAADA WA TZS 9 MIL

 


Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea msaada dawa za meno 2,000 na miswaki 2,000, wenye thamani ya TZS milioni 9 kutoka Kampuni ya Chemi & Cotex, wazalishaji wa dawa ya meno aina ya Whitedent, kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wanaopata huduma katika Idara ya Kinywa na Meno, hususan wenye changamoto mbalimbali za afya ya kinywa na meno.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Dkt. Rachel Mhaville, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji ameishukuru kampuni hiyo kwa kuwakumbuka wagonjwa wenye changamoto za afya ya kinywa na meno, ameongezea kuwa msaada huo utasaidia kuwafikia wagonjwa wanaohitaji, huku akiwataka wadau wengine kuendelea kushirikiana na Muhimbili katika kuboresha huduma za afya.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Chemi & Cotex, Dkt. Erick Sylvester, amesema msaada huo ni mwanzo wa ushirikiano endelevu kati ya kampuni hiyo na Muhimbili. Amesema kampuni hiyo imeamua kutumia nafasi yake kusaidia jamii, hususan katika eneo la afya ya kinywa na meno, kwa kuunga mkono juhudi za taasisi za afya katika kuboresha huduma kwa wananchi.

Msaada huo unatarajiwa kuwasaidia wagonjwa wanaohudumiwa katika Idara ya Kinywa na Meno ya Muhimbili, huku ukiimarisha ushirikiano kati ya sekta binafsi na taasisi za Serikali katika juhudi za kuboresha afya ya kinywa na meno na ustawi wa jamii.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI