Header Ads Widget

ZOEZI LA UPANDAJI MITI ENEO LA SHULE YA MSINGI MBWAMAJI LAONGOZWA NA MWENYEKITI S/MTAA WA MBWAMAJI NDG MAZIKU

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbwamaji Mhe, Yohana Luhemeja akipanda mti eneo litakalojengwa shule mpya ya Msingi Mbwamaji


Na. Mwandishi Wetu, Kigamboni.

MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Mbwamaji uliopo Kata ya Somangira Wilaya ya Kigamboni, Mhe. Yohana Luhemeja 'Maziku' kwa kushirikiana na Wananchi na viongozi wengine wakiwemo Kata, ameongoza zoezi la upandaji miti kwa lengo la kutunza mazingira ya eneo linalotarajiwa kujengwa Shule ya Msingi Mbwamaji.

Zoezi hilo limefanyika leo Mei 9, 2026 eneo la Viwanja vya Dung Farm, Mbwamaji, Ambapo pia viongozi wengine wakiwemo Mtendaji wa Mtaa wa Mbwamaji, Mtendaji wa Kata Somangira, pamoja na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na wadau na Wananchi wamepata kupanda miti ambayo inaenda kuimarisha eneo hilo.

"Tunashukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwezesha Mtaa wetu wa Mbwamaji kupata eneo litakalojengwa shule mpya ya Msingi.

Bi. Belina Zakao Mtendaji wa Mtaa wa S/M Mbwamaji akishiriki zoezi la upandaji miti eneo litakalojengwa shule mpya ya Msingi Mbwamaji.


Miti hii itasaidia kutunza mazingira ya eneo hili na pia itakuwa msaada mkubwa kwa watoto wetu hapo baadae". Amesema Mhe Mwenyekiti Maziku.

Aidha, Maziku amekemea uvamizi wa maeneo ya Serikali katika Mtaa huo na kutoa onyo kali.

"Serikali ya Mtaa Mbwamaji ipo macho, hivyo Sheria kali kwa yoyote atakaevamia haya maeneo.

Katika hatua nyingine, Maziku amewaomba wadau na wananchi kujitokeza kusapoti hatua za awaliza ujenzi wa shule hiyo.

"Kwa sasa tunasubiri hatua za kibali cha Halmashauri ya Wilaya Kigamboni na baada ya hapo tutaanza na nguvu kazi sisi kama Wananchi wa Mbwamaji katika ujenzi wa awali." Amesema Maziku.

Katika tukio hilo, miche ya miti aina tofauti. 300 imepandwa kuzunguka eneo hilo linalotarajiwa kujengwa Shule mpya ya Msingi Mbwamaji.


Mtendaji wa Kata ya Somangira, Bi. Riziki Chaurembo akishiriki zoezi la upandaji miti eneo litakalojengwa shule mpya ya Msingi Mbwamaji



Wadau waliohitokeza kushiriki zoezi la upandaji miti eneo litakalojengwa shule mpya ya Msingi Mbwamaji 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI