Na Mariam Kaagenda _Kagera
Timu 20 za Mpira wa miguu zinazotarajiwa kushiriki Ligi ya Kamachumu Paul Mwijage Cup inayotarajiwa kuanza June 7 Mwaka huu zimepokea vifaa vya michezo pamoja na kanuni za mchezo huo .
Wakati akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari Katibu wa Kamati ya maandalizi ya Ligi ya Kamachumu Paul Mwijage Cup 2026 Bwana Evodius Mariseli Angelo amesema kuwa lengo la Ligi hiyo ni kukuza na kutambua vipaji vinavyopatikana katika Tarafa ya Kamachumu wilaya ya Muleba mkoani Kagera lakini pia na wananchi wa Tarafa hiyo kupata Burudani ya mchezo wa mpira wa miguu.
Amesema kuwa vifaa vilivyotolewa leo kwa timu zote 20 zinazotarajiwa kushiriki Ligi hiyo ni pamoja na mipira ili kuziwezesha timu hizo kufanya maandalizi mapema
Ligi hiyo itazinduliwa rasmi June 7 Mwaka huu siku ya Jumapili ikiambatana na mchezo wa Ngao ya Hisani ambapo Katibu huyo ameongeza kuwa Ligi hiyo itakuwa na Jumla ya Timu 20 na tayari Timu zote zimepata wachezaji na zimeshakamilisha usajili na wamepata vibali vyote vinavyotakiwa.
Kwa upande wao baadhi ya Viongozi wa Timu zitakazoshiriki Ligi ya Kamachumu Paul Mwijage Cup ambao ni Ally Raulenti kutoka timu ya Nyakahama FC, Eshibon Mganyizi timu Mafumbo A wamesema kuwa wamejiandaa vizuri kushiriki Ligi hiyo kwani wana wachezaji wenye uwezo mkubwa wa mchezo wa mpira wa miguu hivyo wameomba marefa wa mchezo huo kutenda haki pindi Ligi itakapoanza.









0 Comments