Header Ads Widget

AG JOHARI KUSHIRIKI WAKILI MARATHONI

 


Chama cha Mawakili wa Serikali nchini, kimeandaa Wakili Marathoni inayolenga kuhamasisha wananchi  ushiriki wa Msaada wa Kisheria wa Mama Samia huduma inayotolewa kwa wananchi wasio na kipato wanaohitaji kupata haki.


Wakili Marathoni inatarajiwa kufanyika jijini Dodoma Mei 30, mwaka huu na kwamba  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Johari amethibitisha kushiriki pamoja na washiriki wengine zaidi ya  5,000 kutoka kada mbalimbali nchini wakiwamo mawakili wa Serikali, wa kujitegemea, wafanyabiashara, watumishi wa umma na wote wenye mapenzi mema na msaada huo.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Serikali, Ado Novemba alisema lengo la Marathoni hiyo ni kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupata haki na stahiki kwa wale wasiokuwa na uwezo bila kutumia gharama.




"Washiriki zaidi ya  zaidi ya 5,000 watashiriki na Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali  amethibitisha kushiriki pamoja na viongozi wengine, watumishi wa umma na Watanzania wote kwa ujumla"alisema Mwenyekiti Novemba.


Kwa upande wake mwanariadha wa zamani Juma Ikangaa kwa niaba ya Rais wa Chama cha Riadha, alisema marathoni ni sehemu ya kuondoa magonjwa yasiyoambukoza ikiwamo Sukari na shinikizo.


Alisema kukimbia ni dawa nzuri kwa watu wote na Kuna faida kubwa, Wakili Marathoni itasaidia afya za washiriki kakama.sehemu na maradhi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI