Header Ads Widget

WANAWAKE TAFORI WAUNGANA NA WENGINE MOROGORO KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


Morogoro, Machi 08, 2026: Wanawake wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) leo wameungana na Wanawake wengine duniani kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa bashasha na shangwe, wakisisitiza umuhimu wa haki na usawa kwa Wanawake na Wasichana katika kufikia maendeleo jumuishi.

Maadhimisho haya yamefanyika katika Viwanja vya Mikese Fulwe, Mkoani Morogoro, yakiongozwa na kauli mbiu isemayo _“Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi Kufikia Dira 2050.”_

Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyowakutanisha Wanawake wa TAFORI na wanawake wengine kutoka taasisi mbalimbali mkoani Morogoro, Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, aliwapongeza Wanawake wa mkoa huo kwa juhudi zao katika maendeleo na uongozi.



Mhe. Malima pia alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake, akisema hatua hiyo inaonyesha nafasi na mchango mkubwa wa mwanamke katika Jamii na Taifa.

“Hili tunalosherehekea leo zamani hata kutajwa lilikuwa haliwezekani, lakini sasa tumepata nafasi ya kusherehekea; tuendelee kuienzi,” alisema.

Aliongeza kuwa Mkoa wa Morogoro unajivunia kuwa kinara katika kuwawezesha Wanawake na kusisitiza kuwa mchango wa Wanawake ni muhimu katika gurudumu la Maendeleo ya Taifa kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Aidha, aliwahimiza Wanawake kutambua kuwa mafanikio yao yapo mikononi mwao na kuwataka kuendelea kushirikiana.

Maadhimisho hayo yamebeba umuhimu mkubwa kutokana na mchango wa Wanawake katika Maendeleo ya Jamii na Taifa, hususan katika Sekta ya Misitu na Ufugaji Nyuki.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI