Header Ads Widget

PROF KABUDI AKUTANA NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA SHIRLEY BOTCHWEY



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Palamagamba Kabudi, amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Shirley Botchwey, yaliyolenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya utawala bora, demokrasia na maendeleo ya pamoja.

Katika mazungumzo hayo, pamoja na mambo mengine, Prof. Kabudi amebainisha kuwa Tanzania inaendelea kuthamini nafasi na mchango wa Jumuiya ya Madola katika kukuza ushirikiano wa kimataifa na kuimarisha taasisi za kidemokrasia. 

Kwa upande wake, Mhe. Botchwey amepongeza ushiriki na mchango wa Tanzania katika shughuli za Jumuiya ya Madola na kuahidi kuendeleza ushirikiano na nchi wanachama.

Mazungumzo hayo yamefanyika jijini London, ambako Prof. Kabudi yuko kwa ziara ya kikazi kushiriki mikutano ya Jumuiya ya Madola inayojumuisha nchi wanachama 56, ikiwemo Kikao cha 72 cha Kamati ya Mawaziri wa Jumuiya ya Madola (CMAG) kitakachofanyika Machi 7, 2026 na Mkutano wa 26 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Machi 8, 2026.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI