Header Ads Widget

POLISI YAFANYA MSAKO, IKIOMBA WENYE TAARIFA ZA WALIOMUUA MFANYABIASHARA WA MADINI


Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia kwa Kamanda wa Polisi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Justine Masejo limetoa wito kwa yeyote mwenye taarifa ambazo zinaweza kusaidia kufanikisha kukamatwa kwa waliohusika na mauaji ya Mfanyabiashara wa madini Abdillah Musa Mollel 'Banjo', kuziwasilisha kwa Jeshi la Polisi ili zifanyiwe kazi.

Kamanda Masejo amebainisha hayo katika taarifa yake kwa Vyombo vya habari leo Ijumaa Februari 20, 2026 ikiwa ni siku moja mara baada ya Jeshi hilo kupata taarifa za Mwili wa mfanyabiashara huyo kuonekana katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma.

"Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha Februari 13, 2026 lilipokea taarifa kuhusu kupotea kwa mtu mmoja aitwaye Abdilah Musa Mollel maarufu kama Banjo na kuanzia hapo tulianza uchunguzi na wakati uchunguzi ukiendelea Tarehe 19, 02, 2026 taarifa zilipokelewa kuwa ameonekana huko Kondoa Mkoani Dodoma akiwa amefariki." Imesema taarifa ya Kamanda Masejo.

Mfanyabiashara huyo wa madini Mkoani Arusha aliyekuwa akiishi eneo la Sanawari Jijini Arusha inadaiwa kuwa mara ya mwisho kuonekana hadharani ni wakati akifanya mazoezi ya mwili kwenye jengo moja katikati ya Jiji la Arusha   na mwili wake umewasili leo Mkoani Arusha na taratibu za mazishi zinafanyika leo nyumbani kwake Sanawari.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI