Header Ads Widget

MGOMO WA DALADALA WATIKISA MOSHI..

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA

MOSHI. 

Daladala zinazofanya safari zake Moshi-Marangu-Kilema, Moshi-Holili na Moshi- Mwika zimegoma kutoa huduma kutokana na kulalamikia kuvurungwa na bajaji zinatoa huduma Himo-Njia panda wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro. 



Mgomo huo ambao umetokea tangu leo asubuhi umesababisha adha kubwa kwa abiria waliokuwa wanasafiri kuelekea maeneo mbalimbali. 

Akizungumza na madereva wa Daladala na Bajaji hao, Mkuu wa wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava aliagiza viongozi wa mamlaka ya usafirishaji nchi kavu (Latra) mkoa kukutana na viongozi wa Daladala na Bajaji kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huo. 


"Nielekeze kwa sasa Bajaji nendeni katika kituo chenu mlichokuwa mmepangiwa hapo awali na ninyi Daladala pia nendeni kwenye kituo chenu endeleeni kutoa huduma wakati vikao vitakaa ili kupata suluhu ya kudumu".

Hadi kufika majira ya saa tano asubuhi bado mgomo huo umeendelea huku wananchi wakipata adha ya usafiri. 

Mwisho.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI