Header Ads Widget

AMANI INATUPA UHURU WA KUJIENDELEZA KIUCHUMI- NIACHIENI


Uwepo wa amani katika Taifa kumetajwa kama miongoni mwa rasilimali muhimu zinazohitajika ili kufanikisha malengo na mipango ya mtu mmoja mmoja, Familia, Jamii na Taifa kwa ujumla, Wito ukitolewa kwa Watanzania kuilinda na kudumisha amani.

Kauli hiyo imetolewa na Bw. Ramadhan Mohamed Niachieni, Mkazi wa Mtaa wa Mkera, Kata ya Msongora Jijini Dar Es Salaam, akisisitiza kuwa amani ndiyo yenye kuleta maendeleo nchini hivyo kila mmoja anawajibika kuilinda kwa ustawi na maendeleo yetu binafsi.

"Amani ina tija sana katika nchi yetu ikiwemo maendeleo ya kila hali kutokana na uhuru wa kufanya shughuli zetu za kiuchumi. Naomba sana tuilinde ili tusiharibikiwe kama wengine na ili tupate fursa ya kuijenga nchi yetu." Amesema Bw. Niachieni.

Mwananchi huyo anaungana na maelfu ya wananchi wengine ambao wamekuwa wakisisitiza kuhusu ulinzi wa amani na kuwakataa wote wenye kuhatarisha amani nchini, wakirejea athari za kiuchumi na kijamii zilizojitokeza wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI