Header Ads Widget

WATENDAJI CCM WAASWA MAADILI,KUJITUMA


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WATENDAJI wa CCM mkoa Kigoma wametakiwa kuzingatia maadili ya utumishi wao, kujituma na kuwa kiungo baina ya viongozi na wanachama wa chama hicho mkoani humo ili kuimarisha utendaji wa chama hicho.

Katibu wa CCM mkoa Kigoma,Christopher Pallangyo alisema hayo katika hafla ya kuwaaga Makatibu wa Jumuia ya wanawake (UWT) mkoani Kigoma na kubainisha kuwa watendaji ndani ya Chama na jumuia zake wanapaswa kuwa na utendaji uliotukuka na kujitenga na makundi yanayoweza kuleta mgawanyiko baina ya viongozi na wanachama wake.

Pallangyo alisema kuwa wakati watumishi hao wanaagwa wapo viongozi,watendaji na wanachama wametokwa machozi na hiyo inadhihirisha kuwa watendaji hao walikuwa kwenye mioyo ya watu na kushirikiana na kila mtu hivyo kuondoka kwao wapo viongozi na wanachama wanaona wamepoteza watu wa msaada kwao.

Akizungumza katika hafla hiyo ya kuwaaga watumishi hao Mwenyekiti wa UWT mkoa Kigoma ,Agripina Buyogera alisema kuwa wamefanya kazi na makatibu hao   ambao  walikuwa kiunganishi kati ya viongozi na wanachama wa jumuia hiyo lakini pia walikuwa kiungo baina ya jumuia hiyo na chama.

Buyogera alisema kuwa wastaafu hao Sarah Kairanya na Asha Kitandala hawakuwa na makundi walifanya kazi na watu wote wakifanya kazi kwa juhudi zilizopelekea kupata ushindi wa kishindo kwenye chaguzi za serikali za mitaa, madiwani, wabunge na Rais ambapo waliwezesha kupatikana kwa idadi kubwa ya viongozi waliochaguliwa kwenye chaguzi hizo.

Akitoa neno la shukrani kwa waalikwa waliohudhuria hafla hiyo Katibu Mstaafu wa UWT mkoa Kigoma,Sara Kairanya alisema kuwa haikuweza kazi rahisi kufanya kazi kwa muda wote na kuondoka bila kuwa na changamoto yeyote na kwamba hiyo inatokana na kuzingatia miongozo ya utendaji, kujituma na uvumilivu hivyo kutaka watendaji wote wa chama na jumuia zake kuvumiliana zinazpotokea changamoto




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI