Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa Elia Kidavile ametoa wito kwa vijana kuzingatia kazi za maendeleo zinazochangia ustawi wa jamii huku akiwataka kuachana na dhana ya siasa kama kazi pekee.
Akizungumza na Matukio Daima Media katika kipindi cha Mpita Njia, Kidavile amesema siasa sio kazi na amewataka vijana kuhakikisha kuwa mbali na majukumu yao ya kisiasa wanakuwa na shughuli nyingine zinazowaingizia kipato na kukuza ustawi wao binafisi na wa jamii.
“Sisi kwenye siasa vijana wengi tumegeuza kama ni kazi ambayo ni ya kutuingizia kipato ilihali sio kweli na sio sahihi kwasababu hata unavyoenda kugombea kwenye hizi nafasi za chama mfano chama chetu cha Mapinduzi kwenye ile fomu wanakwambia kabisa kwamba ujaze kazi unayoifanya kwasababu kile unachoenda kukipambania sio kazi kwahiyo wito wangu mimi kwa vijana ni kuhakikisha kuwa nje ya majukumu ya siasa basi wanakuwa na kazi au ajira ambayo wanaifanya.
Pia ametolea ufafanuzi kuwa ndani ya siasa unaweza kupata kazi lakini hiyo haiwezi kukunyima wewe fursa ya kufanya majukumu yako mengine nje ya siasa huku akijitolea mfano mwenyewe kwa kuwa na ajira yake mwenyewe ambayo anaifanya nje ya siasa.
Kidavile pia ametoa pongezi kwa serikali ya awamu hii chini ya Rais Dkt Samia Suluh Hassan kwa kuazisha Wizara ya Vijana na kusema kuwa serikali imeona mbali sana juu ya jambo hili kwasababu kupitia Wizara hiyo vijana wanayo fursa kubwa ya kueleza changamoto zao.
“Kwanza niipongeze serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt Samia Suluh Hassan kwa kuona mbali na kuazisha Wizara hii ya Vijana, nimekuwa nikiwaambia watu kwamba baada ya uchaguzi huu wa 2025 tutegemee kuwa na Tanzania bora sana na hii imekuwa ni Mfano halisi kwamba Tanzania ya kesho ama ya leo inajengwa na Vijana sasa vijana tunatakiwa tuwe na majukumu maalum tuwe na shughuli maalum za kufanya na ukiangalia Sensa iliyopita asilimia kubwa ya watu katika Tifa hili ni vijana sasa kama vijana tunakuwa hatuna kazi ndipo sasa inakuwa ngumu katika kuchochea maendelo kwa jamii na kwa upande wangu ninaimani kubwa kwamba Wizara hii itakwenda kufanya kazi bora.
Pia ameongeza kuwa ni kweli katika nchi yetu ajira ni changamoto lakini kazi zipo za kutosha cha muhimu ni kuiomba serikali ituwekee mazingira wezeshi na rafiki kwetu sisi ya kufanyia kazi.
Hata hivyo Kidavile amesema kuwa kwa upande wake anaona maono makubwa sana kupitia Wizara hiyo ya Vijana haswa ikiwa na ushirikiano na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwasababu Wizara hizi kwa namna moja au nyingine zinategemeana kwakiasi kikubwa katika kuleta maendeleo katika jamii zetu.
“Mimi nafikiri Wizara hizi mbili zikikaa pamoja na kuwa na Mpango kazi kuna uwezekano mkubwa wa kupata mabadiliko katika jamii zetu hususan kwa haya makundi ambayo yamo ndani ya Wizara hizo Imani yangu ni kubwa sana juu ya utendaji kazi wao.
Pia ametoa maoni yake ambayo Wizara hizi inaweza kufanya ili kuleta mabadiliko kwa jamii akisema kuwa jambo la kwanza kabisa ni kuwasikiliza wananchi wanataka nini japokuwa hicho ndicho ambacho kinafanyika na Wizara hizi na huo ndio utaratibu mzuri wa kujua wanajamii wanachangamoto gani hii itasaidia kwa Wizara kuandaa mpango kazi mzuri.
Hatahivyo Kidavile pia amegusia upande wa Michezo na kutoa pongezi za kutosha kwa Waziri Paul Makonda ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania kwa hamasa kubwa ambayo anaifanya katika sekta hiyo na kusema kuwa wao kama Vijana wanaimani kubwa sana juu yake kwa kuwa atakwenda kuleta mabadiliko mazuri kwao.TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII











0 Comments