Awapongeza Wanafunzi kuripoti shuleni
~ Aridhishwa na upatikanaji wa Chakula Shuleni
Na Matukio Daima Media
Afisa Tarafa Lisekese Emmanuel Shilatu amewapongeza Wazazi, Wanafunzi na Wananchi kwa ujumla kwa hatua na maamuzi ya kuungana na Serikali kuhakikisha Wanafunzi wanaripoti shuleni.
Shilatu ameyasema hayo leo tarehe 14 Januari 2026 wakati akifanya ziara kujiridhisha na hali ya kuripoti Wanafunzi Shuleni ambayo inaridhisha na kufurahisha na kujionea hali ya upatikanaji wa Chakula Shuleni ambapo ameona vyakula na mboga ambazo zipo Shuleni na Wanafunzi wanapata uji na Chakula kwa Shule zote ambapo Leo ametembelea Shule za Msingi, Sekondari na Shule maalum
"Napenda niwapongeze Wanafunzi wote walioripoti Shuleni mapema, nawapongeza Wazazi kuhakikisha kuitikia wito na kuhakikisha Watoto wanapata Chakula Shuleni." Alisema Shilatu
"Kubwa kabisa napenda kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendeleza vyema sera ya elimu bure, kuhakikisha anajenga na kuboresha miundombinu ya Shule ambapo sasa Kuna Madarasa, Madawati ya kutosha na vifaa vya kisasa vya Maabara na uwepo wa Waalimu.
Wananchi waendelee na moyo huo huo wanaoendelea kuuonyesha wa kuungana na Serikali inayoongizwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan." Alisisitiza Shilatu
Akizungumza kwa niaba ya Wazazi waliokuwa Shuleni wakiwapeleka Watoto Shuleni, Iyvone Dihenga ameipongeza Serikali kwa ubora wa miundombinu na kuweka mazingira rahisi kwa Watoto wao kuripoti shuleni na ndio maana wamejitokeza kwa wingi kuungana na Serikali kuwapeleka Watoto Shule.












0 Comments