Header Ads Widget

MATOKEO MAZURI THE GLORY PRIMARY SCHOOL IRINGA YAWAVUTIA WAZAZI



Wazazi wengi mkoani Iringa na maeneo ya jirani wameendelea kuonesha kuvutiwa na shule ya The Glory Primary School baada ya shule hiyo kuendelea kung’ara katika matokeo ya mitihani ya Taifa, hususan ya Darasa la Nne na Darasa la Saba. 

Leo  Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Darasa la Nne na Kidato cha Pili.

Huku wazazi hao wameguswa sana na  matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Nne na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), ambapo shule hiyo imepata matokeo ya juu yanayoitambulisha kuwa miongoni mwa shule bora kitaifa.


Kupitia mtihani wa Taifa wa Darasa la Nne uliofanyika mwaka jana 2025, The Glory Primary School ilishiriki na jumla ya wanafunzi 74. Kati ya wanafunzi hao, wanafunzi 72 wamepata daraja A, huku mwanafunzi mmoja mvulana na mwanafunzi mmoja msichana wakipata daraja B. 

Matokeo hayo yameifanya shule hiyo kuorodheshwa miongoni mwa shule zilizofanya vizuri zaidi nchini, jambo lililozua furaha kubwa kwa wazazi, walimu pamoja na uongozi wa shule.

Kwa mujibu wa wazazi Kefa Sanga na Anna Ndelwa waliozungumza mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, ufaulu huo ni kielelezo cha juhudi kubwa zinazofanywa na shule katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora, yenye misingi imara ya kitaaluma na maadili. 

Wazazi wengi wamesema kuwa matokeo hayo yamewapa imani zaidi juu ya uwezo wa shule hiyo katika kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadaye, ikiwemo kuendelea kufanya vizuri katika mitihani ya ngazi za juu.

Mbali na matokeo ya Darasa la Nne, The Glory Primary School imekuwa ikifanya vizuri pia katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba kwa miaka ya nyuma, hali inayodhihirisha kuwa mafanikio hayo si ya bahati mbaya bali ni matokeo ya mpango madhubuti wa ufundishaji na malezi. 

Walimu wa shule hiyo wameelezwa kuwa ni wenye uzoefu na kujituma, huku wakitumia mbinu za kisasa za ufundishaji zinazomlenga mwanafunzi kikamilifu.

Uongozi wa shule umeeleza kuwa mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mzuri kati ya walimu, wazazi na wanafunzi. 

Pia, shule imewekeza katika mazingira bora ya kujifunzia, ikiwa ni pamoja na madarasa yenye vifaa vya kutosha, vitabu, na programu za ziada zinazosaidia kukuza vipaji na uwezo wa wanafunzi.

Kutokana na matokeo hayo, kumekuwa na ongezeko la wazazi wanaofika shuleni hapo kupata taarifa zaidi kwa ajili ya kuwasajili watoto wao, hasa wale wanaotafuta shule bora yenye rekodi nzuri ya ufaulu na malezi. 

Wazazi wengi wamesema kuwa The Glory Primary School imekuwa mfano wa kuigwa kwa shule nyingine, hasa katika suala la nidhamu, ubora wa elimu na uwajibikaji.

Kwa ujumla, matokeo mazuri ya Darasa la Nne yaliyotangazwa leo yamezidi kuimarisha jina la The Glory Primary School Rungemba Iringa kama moja ya shule zinazoongoza kwa ubora wa elimu nchini, na yameendelea kuwavutia wazazi wengi wanaotamani kuwaona watoto wao wakifanikiwa kielimu na kimaadili.

WASILIANA NA THE GLORY PRIMARY SCHOOL

0745 144 141

0744 333 311

0745 150 505

TAZAMA ZAIDI BOFYA LINK HII

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI