Header Ads Widget

DKT. KIJAJI AHIMIZA KAZI NA UTU*




 Dodoma

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, amezitaka Taasisi zilizoko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Utu pamoja na kuishirikisha  jamii katika shughuli za uhifadhi na Utalii.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Leo tarehe 15 Januari 2026, jijini Dodoma alipokuwa akifunga kikao kazi maalum cha siku mbili kilicholenga kupitia taarifa za utekelezaji wa majukumu ya taasisi za Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Aidha amewapongeza viongozi hao kwa kusimamia vyema shughuli za uhifadhi na Utalii hali inayoonesha kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za uhifadhi na Utalii endelevu kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla

Akifunga kikao hicho Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Chande (Mb) amehimiza utendaji unaozingatia teknolojia ili kuzipatia suluhu changamoto zinazosababishwa na migogoro baina ya binadamu na wanyamapori ili kufikia azma ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuleta tabasamu kwa wananchi anaowaongoza. 

Kikao hicho  kimeudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Utalii Bw. Nkoba Mabula na Managementi ya Wizara, Watendaji na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara na Maafisa wengine wa juu wa Wizara hiyo yenye dhamana ya uhifadhi na Utalii nchini.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI