Wanaharakati Mange Kimambi na Maria Sarungu Tsehai wenye msururu kadhaa wa lawama, malalamiko na kutajwa kuwa sababu ya uvunjifu wa maadili, amani na umoja wa Watanzania wamefungiwa akaunti zao za Meta, kampuni mama ya Teknolojia yenye kumiliki mitandao ya (Instagram, Facebook na WhatsApp).
Mange na Maria wanashutumiwa pia kwa kuchochea matukio ya uvunjifu wa amani, mabaya zaidi kuwahi kutokea kwa siku za hivi karibuni nchini Tanzania, Yakifanyika wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali za umma na za binafsi, Wizi, uchomaji moto na vifo vya watu kadhaa kulikotokana na udhibiti wa tukio hilo na umiliki wa silaha kutoka kwa Vituo vya Polisi vilivyovamiwa na Makundi hayo ya kihalifu.
Meta imethibitisha taarifa hizo kwa kuandika " Akaunti hizo zimeondolewa kwa kukiuka sera yetu. Haturuhusu watu kuunda akaunti mpya zinazofanana na zile tulizoziondoa awali kwa kukiuka viwango vya juu vya Taasisi ya Meta."
Mange na Maria wanatajwa kupokea mabilioni ya fedha kutoka kwa Taasisi na watu binafsi ili kuchochea vurugu, chuki na machafuko ndani ya Tanzania, wakitumia mitandao yao ya Kijamii kuratibu na kuhamasisha machafuko na mauaji ya raia nchini Tanzania kwa kipindi kirefu hivi sasa suala ambalo limesababisha wananchi wa Tanzania kufurahishwa na uamuzi wa @meta kuzifungia akaunti zao kwa mustakabali wa amani na ulinzi wa haki za binadamu.
Watu hawa wamepigiwa mfano kama watu halisi wanaotumia Mitandao ya Kijamii kwa namna hasi yenye kuleta hasara, ghasia na vurugu kwenye jamii kwa maslahi yao binafsi bila kujali haki za wengine.
Hii si mara ya kwanza kwa Kampuni ya Meta kuzifungia akaunti zinazokiuka miongozo ya kampuni hiyo ya teknolojia kwani Januari 2021, Meta waliifunga akaunti ya X ya Rais wa Marekani Donald Trump kwa kile walichokieleza kama hatari ya kuchochea vurugu baada ya kutoa wito kwa wafuasi wake kuvamia bunge wakijaribu kuvuruga kikao cha kuidhinisha ushindi wa Rais Mstaafu Joe Biden. Vurugu hizo zilifanyika na zilisababisha uharibifu na vifo kadhaa vya wananchi.
Aidha mwaka 2022 Mtandao wa X pia ulizifungia akaunti za gazeti maarufu nchini humo la Caravan na akaunti ya muigizaji Sushant Singh na ya Mwanaharakati Hansraj Meena kwa madai ya kukiuka masharti ya mtandao huo kutokana na kujihusisha na maandamano ya kutaka mabadiliko katika kilimo nchini humo.








0 Comments