NA CHAUSIKU SAID MATUKIO DAIMA.
Wakulima wa zao la pamba Wilaya ya Kishapu, Mkoani Shinyanga wamepata msukumo mkubwa katika uzalishaji wa zao hilo baada ya serikali kupitia Bodi ya Pamba kutoa Matrekta 19 yaliyoleta mabadiliko chanya katika kilimo ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza tija na kuwasaidia wakulima kulima kwa ufanisi zaidi.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Peter Masinda ameeleza kuwa matrekita hayo ni nyenzo muhimu katika kuboresha uzalishaji wa zao la pamba na wananchi wa Wilaya hiyo wanategemea kilimo hicho kama zao kuu la kibiashara, kwani linakabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo changamoto za ukame na mvua chache.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Peter Masinda akielezea uzalishaji wa zao la pamba umeongezeka mara mbili zaidi ya miaka mingine iliyopita na matarajio yao katika msimu huu wa Mwaka 2025/2026 ni Kuongeza tija katika uzalishaji baada ya wakulima kutumia matrekita kulima.
“Matrekta haya ni msaada mkubwa kwa wakulima wetu hata uzalishaji umeongezeka mara mbili zaidi ya miaka mingine iliyopita na matarajio yetu katika msimu huu wa Mwaka 2025/2026 ni Kuongeza tija katika uzalishaji kwani kipindi Cha nyuma walikuwa wanatumia mbinu za jadi katika kulima ambazo zilikuwa zikifanya kazi kwa viwango vya chini, Lakini sasa, kupitia matrekta haya , yanaweza kuleta tija na mabadiliko katika uzalishaji wa zao la pamba,” alisema Masinda.
Masinda ameongeza kuwa matrekta hayo si tu nyenzo za kuboresha kilimo, bali ni uwekezaji wa kudumu katika maendeleo ya kilimo cha pamba hivyo yamekuwa chachu katika kuongeza uzalishaji, pia wanatarajia kuona tija kubwa zaidi katika msimu huu wa kilimo.
“Uwepo wa matrekta haya utasaidia wakulima kuzalisha pamba kwa wingi na kwa ufanisi zaidi. hii itaongeza kipato cha wakulima na kuchangia katika uchumi wa wilaya yetu na taifa kwa ujumla,” alisema Masinda.
Afisa kilimo Wilaya ya Kishapu kutoka Bodi ya Pamba Joachim Gobanya akielezea uwepo wa matrekita katika Wilaya ya kishapu wakulima wameweza Kuongeza tija katika kilimo cha pamba kwa kupunguza gharama za kilimo na kuongeza uzalishaji kwa kila ekari.
Afisa kilimo Wilaya ya Kishapu kutoka Bodi ya Pamba Joachim Gobanya amesema kuwa matrekita hayo yamewasaidia wakulima hadi sasa wameishaandaa hekta 1,360 na wanatarajia zaidi ya hekta 20,000 huku Trekta moja linalima hekta 10 au zaidi kwa siku, na zimesambazwa katika kata za Wilaya hiyo.
Hata hivyo Gobanya ameeleza kuwa matrekta hayo yametumika kufungua maeneo mapya ya kilimo na kusaidia wakulima kulima kwa mpangilio na Kuongeza tija katika kilimo cha pamba kwa kupunguza gharama za kilimo na kuongeza uzalishaji kwa kila ekari.
"Awali, wakulima walikuwa wanapata kilo 200 za pamba kwa ekari moja, lakini baada ya matrekta haya kuletwa, wakulima sasa wanapata hadi kilo 1200 kwa ekari moja hii ni tofauti kubwa na inadhihirisha jinsi matrekta yanavyoweza kuboresha uzalishaji," alisema Gobanya.
Matrekta hayo yanasaidia kupanda pamba kwa mpangilio lakini kupalilia shamba kwa ufanisi, na kufanya shughuli za kilimo kuwa rahisi na za haraka pia inasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wao, licha ya changamoto za hali ya hewa kama ukame na mvua chache.
Afisa kilimo BBT Gaudi Tungalaza kutoka kata ya shagihilu akielezea namna ambavyo wameweza kutoa elimu Kwa Kwa wakulima na kuweza kulima kilimo chenye tija.
Steven Timotheo, Mkulima kutoka Kijiji cha Shagihilu Wilaya ya kishapu ameeleza kuwa baada ya kupata matrekta hayo yaliyoleta na serikali kupitia bodi ya pamba wakulima wakulima wamepata mwitikio wa kulima na kuzalisha Kwa tija wakati hapo nyuma walikuwa wanapata hasara walipokuwa wakulima Kwa kutumia mbinu za kilimo za kizamani, lakini kwa sasa, matrekta yameleta mabadiliko makubwa katika kilimo cha pamba.
" Kipindi Cha nyuma kulima pamba ilikuwa ni changamoto sana, tulikuwa tunalima kwa mikono na majembe ilikuwa inachukua muda mrefu na ilikuwa inahitaji nguvu nyingi. Lakini sasa na matrekta, tunafanya kazi kwa haraka na kwa ufanisi. Hekari moja inayolimiwa na trekta inaleta tija kubwa, na wakulima wanavuna zaidi kuliko walivyokuwa wanavuna awali,” alisema Timotheo.
Ameeleza kuwa trekta zinazotolewa na serikali zinatulimia kwa bei ya ruzuku (shilingi 35,000 kwa ekari) zinasaidia wakulima wengi ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matrekta binafsi ambazo zinatulimia Kwa elfu 50000 mpaka 60000 lakini pia tunaishukru Bodi ya pamba Kwa na maafisa ugani kwa elimu waliyotupatia mpaka tumeweza kupata mavuno ya kutosha
Mkuu wa Wilaya ya kishapu amehitimisha Kwa kuomba serikali kuwaongezea wakazi wa Wilaya hiyo mbegu za kutosha, matrekita kutoka 19 hadi 60 kwa vijiji 117, na miundombinu ya umwagiliaji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuongeza uzalishaji wa taifa.
0 Comments